Beki wa Manchester United anayetoka Ivory Coast Eric Bailly alipata jeraha mbaya ya goti wakati wa mechi ambayo timu yake ililazwa 4-0 na Chelsea jana Jumapili.
Mchezaji huyo wa miaka 22 aliumia baada ya kukabiliana na Eden Hazard wa Chelsea.ALiondolewa uwanjani dakika ya 52.
Bailly alikuwa amechezea United mechi zote walizocheza msimu huu ligini. Alijiunga nao kutoka klabu ya Villarreal ya Uhispania kwa £30m kabla ya kuanza kwa msimu.