majadiliano ya amani yazidi kuzorota- Afghanistan

Mjumbe wa ngazi ya juu wa majadiliano ya amani auwawa Afghanistan

Watu wenye silaha wamempiga risasi na kumuua mjumbe wa ngazi ya juu wa majadiliano ya amani na kiongozi wa zamani wa Taliban mjini Kabul jana Jumapili,
katika pigo jingine katika juhudi za Afghanistan za kumaliza mapigano yaliyodumu kwa muongo mmoja sasa ya kundi la Taliban. Arsala Rahman , mjumbe wa baraza la juu la amani aliuwawa katika tukio la kushambuliwa na watu waliokuwa katika magari wakati akiwa njiani kwenda ofisini kwake katika eneo la kaskazini ya mji mkuu Kabul.
Rahman ni mjumbe wa pili wa ngazi ya juu wa baraza hilo lililoundwa na rais Hamid Karzai kuuwawa katika muda wa chini ya mwaka mmoja. Burhanudin Rabbani ,
rais wa zamani wa Afghanistan na kiongozi wa baraza hilo la juu la amani , aliuwawa katika shambulio la kujitoa muhanga nyumbani kwake Septemba mwaka jana.

-DW