Majadiliano Muswada wa Habari Bungeni

Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini, Zitto Kabwe akichangia hoja bungeni Dodoma,  kuhusu Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016, ambapo alisema kuwa muswada huo hauwatendei haki wanahabari.

Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini, Zitto Kabwe akichangia hoja bungeni Dodoma,  kuhusu Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016, ambapo alisema kuwa muswada huo hauwatendei haki wanahabari.

Mwenyekiti wa Jukwaa la Habari Tanzania (TEF), Theothil Makunga (kulia), akiwa na wajumbe wa jukwaa hilo, Jane Mihanji (katikati) baada ya kutoka bungeni Dodoma , kusikiliza mwenendo wa majadiliano ya Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari.

Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge akiongoza majadiliano hayo

 

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akiwasilisha bungeni Dodoma, Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akipongezana na naibu wake, Anastazia Wambura baada ya kuwasilisha muswada huo

 

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye (katikati) akijadiliana jambo na Mjumbe wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEA), Jane Mihanji (kulia) na Saedy Kubenea kwenye viwanja vya Bunge, Dodoma, baada ya kuwasilisha Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari.

Waziri Kivuli wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Joseph Mbilinyi akiwasilisha bungeni, Dodoma maoni ya Kambi rasmi ya Upinzani kuhusu Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016

 

Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Saedy Kubenea akichangia muswada huo