Afrika Kusini,
RAIA mmoja wa Afrika Kusini ameamka na kujikuta yupo kwenye chumba cha kuhifadhia maiti mwishoni hivi karibuni, na kuanza kupiga kelele akitaka wahudumu wa chumba hicho wamtoe huku wao wakihofu na kudhani ni mzimu.
Familia ya mtu huyo iliamua kutoa taarifa mochwari baada ya kudhani amekufa kwa kile kushindwa kumwamsha Jumamosi usiku na hivyo kuwasiliana na ofisi moja yenye vyumba vya kuhifadhia maiti ya mtu binafsi katika kijiji kimoja mjini Eastern Cape, kwa ajili ya kuchukua mwili na kuuifadhi.
Mtu huyo alikaa kwenye chumba hicho cha kuhifadhia maiti kwa muda wa saa 24, msemaji wa idara ya afya mjini humo aliliambia shirika la habari la mjini Sapa.
Wahudumu hao baadae walirejea na kupiga simu kuita gari la wagonjwa ili kupelekwa hospitalini kwa vipimo zaidi. Mtu huyo ambaye jina lake limehifadhiwa, alitibiwa hospitalini kwa kukosa maji mwilini.
Msemaji wa idara ya afya ya Eastern Cape Sizwe Kupelo alisema, “Daktari walimfanyia uchunguzi na kuona kuwa anaendelea uzuri.”
“Hakuhitaji matibabu ya ziada.” Kupelo alisema mtu huyo aliamka saa tisa za Afrika Mashariki siku ya Jumapili, akitaka kutolewa kwenye chumba hicho chenye baridi kali kwenye kijiji cha Libode, na kuwatisha wahudumu waliokuwa zamu.
Kupelo alisema, “Mwanzo watu hao walikimbia kwa kasi.” Maofisa wameusihi umma kuwasiliana na madaktari au wanaotoa huduma za dharura ili waweze kumtangaza mtu kufariki dunia kabla ya kuwaita wahudumu wa vyumba vya kuhifadhi maiti. Kupelo alisema, “Unaanza kujiuliza ni watu wengine wangapi waliokufa kwa namna hiyo katika chumba cha kuhifadhia maiti.”
-BBC