Maelfu ya watu wamehudhuria swala ya kiislamu ya kumuombea aliyekuwa mwandondi bingwa duniani Muhammad Ali ambae alikufa wiki iliyopita.
Swala hiyo imefanyika katika ukumbi wa ‘Freedom Hall’ katika mji aliokulia wa Louisville.Waombolezaji walisikika wakimpa sifa Muhammad Ali kwa kuulita jina lake wakati mwili wa bondia huyo ulipoingizwa ukumbini.
Viongozi wakubwa katika ulimwengu wa ndondi na wanaharakati walikuwa sehemu ya waliohudhuria.Swala imeongozwa na Imam wa California, sheikh Zaid Shakir, ambae alikuwa pembezoni mwa Muhammad Ali pindi alipokuwa anakata roho na kupata fursa ya kumwombea dua ya mwisho kabla ya maziko.
Itakumbukwa kuwa, ukumbi wa Freedom Hall ndio sehemu ambayo pambano la mwisho la Muhammad Ali lilifanyika.Wakati huo huo , serkali ya kongo kinshasa imepanga kufanya sherehe rasmi ya kumkumbuka mwanandodi huyu ambae alipambana dhidi GEROGES FOREMAN mwaka 1974, inchini humo kwa mwaliko wa aliyekuwa rais wa nchi hiyo Mobutu Seseko.