Yohane Gervas, Rombo
VIONGOZI wa dini wameshauriwa kuwaongoza waumini wao kuhuburi Amani na kujiepusha na migogoro kwani migogoro haina tija yeyote. Ushauri huo umetolewa na Msaidizi wa Kisheria wa Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es salaam wakati alipokuwa akihutubia katika jubilee ya Miaka 75 tangu kuanzishwa kwa Kanisa la Tanzania Assembys of God [TAG] iliyofanyika katika Kanisa la Jerusalemu usharika wa Mkuu seksheni ya Rombo.
Alisema kuwa siku za hivi kaibuni kumeibuka migogoro mbalimbali inayowahusisha viongozi wa kidini ikiwemo kugombania mali za kanisa au vyeo jambo ambalo amesema kuwa linajenga picha mbaya katika jamii.
Mramba amesema kuwa viongozi wa dini wanatakiwa kuwa mfano wa kuigwa katika kuhubiri Amani kwani wao ni mabalozi wa Yesu Kristo wa kuhubiri Amani. Aidha amewataka kutumia njia za usuluhishi za kutatua migogoro badala ya kupelekana mahakamani jambo ambalo jamii inapoteza imani na viongozi wao. Pia viongozi wa dini wametakiwa kuacha ushabiki wa kisiasa wa namna yoyote.