Na Magreth Kinabo – MAELEZO
MAHAKAMA ya Rufani Tanzania itasikiliza jumla ya kesi 33 zinazohusu watu mbalimbali. Kesi hizo ambazo ni za madai na makosa ya jinai zitaanzwa kusikilizwa kuanzia Februari 13, mwaka huu hadi Machi 5, mwaka huu mkoani Arusha.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Naibu Msajili wa John Mgetta Mahakama ya Rufani Tanzania ilieleza kuwa kesi hizo zitasikilizwa na majaji watatu, ambao ni Jaji Eusebia Munuo, Engela Kileo na William Mandia.
Taarifa hiyo ilizitaja baadhi ya kesi kuwa kesi namba 22/2011 inayohusu Leonard Kilasi na wenzake 549 dhidi ya kampuni ya DECI Tanzania. Kesi hizo zitatolewa hukumu Machi 5, mwaka huu.