HATIMAYE Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imelifukuza mahakamani ombi dogo la Mwandishi wa Habari, Saed Kubenea lilokuwa likiiomba Mahakama hiyo itoe amri ya zuio la muda la kulizuia Bunge Maalum la Katiba linaloendelea na vikao vyake Dodoma lisiendelee na vikao vyake hadi Kesi ya Msingi aliyofungua mahakamani hapo itakaposikilizwa na kuamriwa.
Uamuzi huo umetolewa Leo na jopo la Majaji wa Tatu Agustine Mwarija, Dk. Fauz Twaibu na Alocye Mujulisi ambayo walisema ombi Hilo dogo Na.29/2014 ambalo mlalamikaji ni Kubenea dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa serikali, lilifunguliwa mahakamani hapo pamoja na Kesi ya Msingi Na. 28/2014 ambayo lilifunguliwa na Kubenea dhidi ya AG.
Jopo hilo lilisema walianza kusikiliza ombi dogo la Kubenea lakini AG ambaye aliwakilishwa na Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju waliwasilisha pingamizi na kutaka ombi hilo dogo litupwe kwasababu lina dosari za kisheria.
Masaju alitaja moja ya dosari ya ombi hilo la Kubenea ni kwamba alitumia kifungu cha 2.2 cha Sheria inayoruhusu matumizi ya Sheria nyingine (Judicature and application of Laws Act) (JALO). Kifungu ambacho siyo sahihi kwani JALO ilifanyiwa marekebisho na baada ya kufanyiwa marekebisho Sheria hiyo hivi sasa inaitwa JALA na hivyo Kubenea alipaswa alete ombi lake hilo chini ya Kifungu Cha 2.3 nchi JALA na siyo Kifungu Cha 2.2 cha JALO.
Jopo hilo lilikumbusha kuwa kesi hiyo jana ilikuja kwa ajili ya Mahakama kutoa uamuzi wa mabishano Hao ya kisheria kuhusu uhalali wa ombi Hilo dogo na kwamba Mahakama hiyo Imefikia uamuzi wa kukubaliana na pingamizi la Wakili wa mdaiwa, Masaju Kuwa Kubenea alitumia Kifungu kisicho sahihi Kuwasilisha ombi Hilo mahakamani hapo na kwasababu hiyo Mahakama hiyo imelifukuza/tupilia Mbali ombi la Kubenea na Kesi ya Msingi itaanza kusikilizwa Kesho Kutwa.
Na kwa uamuzi huo wa mahakama, Bunge Maalum la Katiba linaendelea na vikao vyake kwa mujibu wa Ratiba iliyokuwa limejiwekea. Hata hivyo Kubenea hakuwepo mahakamani hapo leo.
Chanzo: Facebook: Happy Katabazi