Mahakama Arusha Yatengua Ubunge wa Longido

kadogooo11111

Mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Arusha imetengua ushindi wa aliyekuwa mbunge wa Longido ,Onesmo Nangole kuwa mbunge wa jimbo la Longido kupitia chadema kutokana na kukiuka taratibu za uchaguzi

Akisoma Hukumu hiyo jana , Jaji mfawidhi wa kanda ya Bukoba Sivangilwa Mwangesi ,alisema mahakama imeamua kubatilisha matokeo ya uchaguzi kutokana na kuweko kwa kasoro zilizopelekea mahakama kuona kulikuwepo na mpango wa uovu kwenye matokeo

Akitaja kasoro hizo alisema ni kuingiza fomu ambazo si stahiki wakati wa kuhesabu kura ,kufanya fujo kwenye chumba cha kuhesabia kura,kutolewa kwa mlalamikaji nje na wakala wake wakati zoezi la kujumuisha kura likiendelea ,kutangaza matokeo pasipo mlalamikaji kuwepo

Hata hivyo alisema fomu ambazo zilikuwa za uchaguzi wa madiwani zilitumika kuingiza matokeo wakati wa majumuisho ya kuhesabu kura kinyume na matakwa na hakuna taarifa yeyote iliyotolewa juu ya uwepo wa fomu hizo

“Fomu 21 (c) ilingizwa kinyume na taratibu na baada ya kuona ni kosa alihaririwa na kuandikwa fomu 21 (b) kitu ambacho mahakama imetilia ulakini juu ya uwepo wa fomu hiyo ,”alisema Sivangilwa

“Hata hivyo alisema alipouliza mshatikiwa wa 3 ambaye ni msimamizi wa uchaguzi hakuweza kutoa taarifa kamili iliyoonesha mahakama kuwa hapakuwa na kasoro,”alisema Jaji Sivangilwa

“Mahakama imeona kuingizwa kwa fomu zisizostahili inaashiri kulikuwepo na lengo la kudanganya na kutoposha ukweli wa maamuzi ya wapiga kura ,”alisema Jaji Sivangilwa

Pia alisema kutokana na mlalamikaji Dk.Steven Kiruswa kupitia CCM kutoa malalamiko ya kufanyiwa fujo na malalamikiwa Onesmo Nangole na wafuasi wake kwenye chumba cha kufanyia majumuisho ya kura ,pamoja na kuthibitishwa na polisi kuwepo na vurugu mahala hapo ,imedhihirisha kuwa kulikuwepo na mpango wa uovu juuu ya kubatilisha matokeo hayo

Pia mahakama ilitupilia mbali hoja ya mlalamikaji kutolewa lugha za kibaguzi na Onesmo Nagole na wafuasi wake na kusema hizo zilikuwa ni siasa maji taka zisizokuwa na madhara ya kudumu

Pia ilitupilia mbali shauri la kuwepo kwa magari ya chadema na usindikizwaji wa masunduku ya kupigia kura ambako chadema walituhumiwa na kusema mlalamikaji hakuweza kudhibitisha juu ya malalamiko yake

Pamoja na hayo ,Jaji mfawidhi alitengua ushindi wa mbunge huyo na kutaka uchaguzi urudiwe ikiwa ni pamoja na kuagiza fidia kulipwa kwa mlalamikaji

Upande wa mlalamikiwa wa kwanza Onesmo Nangole alisema atakataa rufaa juu ya hukumu ya kesi hiyo kwakua mahaka haijamtendea haki

Wakili wa utetezi wa Nangole ,John Materu alisema wanasubiri nakala ya hukumu kutoka kwa jaji ili waakate rufaa

Upande wa mshindi wa kesi hiyo Dr Steven Kiruswa alisema ameridhika na hukumu hiyo kwakua alitumwa na wapiga kura kuja kudai haki yao

Mwenyekiti wa mkoa wa chama cha mapinduzi Micheal Lekule Laizer alitoa ujumbe kwa aliyekuwa mbunge huyo ,akubali kushindwa na warudi wenye uchaguzi tena

Onesmo Nangole kupiti achama cha demokarsia maendeleo alitangazwa mshindi kwa kura 20,076 ,huku mshindi wa pili akiwa ni Dk Steven Kiruswe akiwa na kura 19,352.

Kesi hiyo Dk.Steven aliwashitaki ,Mgombe mwenza Onesmo Nangole ,Mwanasheria mkuu wa serikali pamoja na msimamizi wa uchaguzi longido