Mahafali ya Chuo Kikuu Cha Dodoma Katika Picha Anuai

Wahitimu wa Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) Wakiwa na nyuso za Furaha mara baada ya kutunukiwa shahada zao katika mahafali ya tatu ya Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) yaliyofanyika Novemba 22, 2012 katika viwanja vya Chimwaga.

  Naibu Makamu Wa Mipango, Utawala na Fedha wa Chuo Kikiku cha Dodoma  Prof. Shaaban A. K. Mlacha akiongoza maandamano ya elimu Katika Sherehe za Mahafali ya Tatu ya Chuo Kikuu Cha Dodoma yaliyofanyika tarehe 22 Novemba 2012 Huku akifuatiwa na Mkuu Wa Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM), Benjamin Mkapa.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) Prof Idris Kikula akisoma hotuba mbele ya Mkuu Wa Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM), Benjamin Mkapa (Hayupo Pichani) katika mahafali ya tatu yaliyofanyika tarehe 22 Novemba 2012
Mkuu Wa Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM), Benjamin Mkapa akimtunuku Mhitimu wa Shahada ya Uzamivu Mmoja kati ya wahitimu wa tatu wa shahada ya juu kabisa ya Uzamivu ya Chuo Kikuu Cha Dodoma katika mahafali ya tatu ya Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) yaliyofanyika tarehe 22 Novemba 2012.
Mmiliki wa Lukaza Blog (Wa Pili Kushoto) akiwa katika picha ya kumbukumbu na baadhi ya wahitimu wa Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) katika mahafali ya tatu ya Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) yaliyofanyika viwanja vya chimwaga tarehe 22 Novemba 2012.

Baadhi ya Ndugu, Jamaa na Marafiki wa wahitimu waliohudhuria mahafali ya tatu ya Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) yaliyofanyika tarehe 22 Novemba 2012 katika Viwanja Vya Chimwaga . PICHA ZOTE NA JOSEPHAT LUKAZA WA LUKAZA BLOG.