Magonjwa Sugu ya Ini na Upandikizaji Wake

Magonjwa Sugu ya Ini na Upandikizaji
INI pamoja na kuwa chombo kikubwa katika mwili wa binadamu pia ni kiungo muhimu kwa ajili ya kazi za kimwili kwa maana iyo ni vigumu kwa mtu kuishi bila Ini.
Kutokana na maendeleo katika mbinu za kisasa za upasuaji, kwa sasa upasuaji unafanyika kwa watu wengi zaidi kuliko miaka ya nyuma kwa kuwa watu wengi wako tayari kufanyiwa upasuaji kutokana na kuboreshwa kwa viwango vya mafanikio ya upasuaji.
Maradhi sugu ya Ini yanaweza kusababisha mtu kuhitaji upandikizaji ambao kwa kawaida unapendekezwa kwa watu walio kwenye hatua ya mwisho za magonjwa ya Ini (ESLD – End Stage Liver Diseases).
Ini linawajibika kwa kazi kadhaa muhimu za mwili kama vile kubadilisha chakula kuwa nishati na kusafisha damu kutokana na sumu na madawa ya kulevya. Kiungo hiki pia kina uwezo mkubwa wa kubeba damu, kwa wakati mmoja ina uwezo wa kua na karibu asilimia 13 ya damu ya mwili.
Miongoni mwa magonjwa yanayoathiri Ini ni pamoja na homa ya manjano, saratani, ugonjwa sugu wa mirija ya Ini (cirrhosis) ambao pia ni mchangiaji mkuu katika kusababisha mtu kuitaji upandikizaji. Haya pia ni miongoni mwa orodha ya magonjwa sugu ambayo hatua kwa hatua yanakuwa mzigo kwa kiwango cha kimataifa.
Kulingana na shirika la afya duniani inakadiriwa 46% ya magonjwa na 59% ya vifo ni matokeo ya maradhi sugu. Katika mtazamo mwingine inasemekana kuwa watu milioni 35 wanaokufa kila mwaka ni waathirika wa ugonjwa sugu na takwimu zinaongezeka.
Kimataifa magonjwa ya Ini yanashika nafasi ya tano kwakusababisha vifo yakiwa nyuma ya kansa na magonjwa ya moyo, kiharusi na ugonjwa wa kifua. Hata hivyo watafiti wanasema kuwa tofauti na magonjwa mengine kiwango cha vifo vya magonjwa ya ini yanaongezeko badala ya kupungua. Kwa Tanzania miongoni mwa magonjwa ya kuambukiza zaidi ni Homa ya Manjano A na Homa ya Manjano E (Hepatitis A and Hepatitis E). Yote ni magonjwa yanaosababishwa na virusi huenea kwa maji machafu au chakula na kuingilia utendaji kazi wa ini.
Virusi pia ni mtesaji mkuu kwa kiwango cha kimataifa, katika yote Homa sugu ya manjano ni mchangiaji vifo 1.3million duniani kote takwimu ambazo zinalinganishwa na mzigo wa TB, VVU / UKIMWI na malaria.
Upandikizaji wa Ini unahusisha kubadilisha Ini lenye ugonjwa na Ini zima au sehemu ya Ini zima kutoka kwa mtu mwingine. Kwa sasa hakuna mashine ambayo inaweza kuiga kazi ya Ini utaratibu huu hatari unafanywa tu kama kuna ukosefu wa tiba nyingine.
Pamoja na kiwango cha mafanikio yake ya hivi karibuni utaratibu huu una uwezekano wa kusababisha kifo kutokana na matatizo wakati na baada ya tukio hilo.
Dk. Anand Khakhar Mshauri Mwandamizi wa upandikizaji na Upasuaji wa Ini na Mkurugenzi Programu ya Kupandikiza Ini katika Kituo cha Magonjwa ya Ini na Upandikizaji, Hospitali za Apollo, Chennai, India anasema kwamba “kuna mbinu 3 za upandikizaji Ini: upandikizaji kutoka kwa maiti, upandikizaji kutoka kwa mtu hai na upandikizaji aina ya tatu ni upandikizaji wa sehemu ya ini ambao haitumiki mara kwa mara. Katika upandikizaji kutoka kwa maiti Ini la mtoaji linachukuliwa kutoka kwa mtu ambaye amegundulika amekufa, ambaye familia yake imejitolea kuchangia ogani kwa ajili ya upandikizaji. Watu ambao wanatakiwa kufanyiwa upandikizaji kutoka kwa maiti husubiri katika orodha ya taasisi/kanda mpaka wapatikane wafadhili wanaofaa.”
“Kupandikiza kutoka kwa mtoaji Hai inahusisha mwanafamilia mwenye afya, kwa kawaida mzazi, ndugu, au mtoto, au mtu wa karibu kihisia, kama vile mke, kujitolea kuchangia sehemu ya Ini kwa ajili ya upandikizaji. Mfadhili anatathminiwa kwa makini na timu inahakikisha hakuna madhara yanayoweza kutokea kwa mfadhili au mpokeaji.”
“Upandikizaji wa msaada unahusisha sehemu ya ini ya mtoaji mtu mzima mwenye afya (hai au maiti) kupandikizwa kwa mpokeaji. Ini la mgonjwa linabaki kama lilivyo mpaka kipande kisaidizi kinapoanza kufanya kazi. Ini lenye ugonjwa linaweza sasa kuondolewa.”
Mapema mwezi huu timu ya madaktari kutoka Hospitali ya Apollo , Kituo cha Magonjwa ya Ini na Upandikizaji (CLDT) wakiongozwa na Dk. Anand Khakhar na Dr Anil Vaidya wamefanikiwa kufanya “Multi-Visceral” ya pili kwa wagonjwa wengi kwa hisani ya maiti ya mtu.
Kupandikiza Ini ambako ni kawaida hufanyika kwa mpokeaji mmoja, lakini mara kadhaa hugawanywa kusaidia mtu mzima na mtoto, katika tukio hili pia liligawanyika kwa watu wazima wawili, ushirikiano ambayo ni mara chache kufaniikisha.
Kwa kufanya hivyo hospitali hii inakuwa ya kwanza kufanya operesheni hiyo nchini India kwa mtu anayeteseka kwa tumbo kushindwa kufanya kazi vizuri tangu utotoni. Kesi hii pia ilikuwa ya kwanza ambapo ukuta wa tumbo ulipandikizwa juu na katika matumbo ili kuondoa tofauti kati ya mtoaji na mpokeaji wa matumbo.
Kuhusu Kitengo cha upandikizaji wa Ini katika Hospitali za Apollo.
Huduma upandikizaji wa Ini katika Hosipitali ya Apollo inalenga kutoa huduma kwa ufanisi kwa wagonjwa wa ini. Upandikizaji Ini wa mafanikio, unaotolewa katika hospitali za Apollo ni wa uhakika.
Hospitali za Apollo zina Kitengo kikubwa sana cha upandikizaji wa Ini nchini India chenye mpango madhubuti wa uhifadhi na upatikanaji wa Ini kwa ajili ya upandikizaji
Hospitali za Apollo zilizopo Delhi, Chennai, Hyderabad, Kolkata, Ahmedabad na Bangalore hutoa upasuaji na upandikizaji wa ini na ndivyo vinavyofanya kuwa mtandao mkubwa wa upandikizaji wa ini nchini India.
Hospitali ya Apollo ya Indraprastha, iliyopo mjini Delhi imefanikiwa kufanya upandikizaji wa ini kwa wagonjwa 200 kutoka Pakistan Novemba 2011.
Kwa kiwango cha zaidi ya asilimia 90% kupitia mafanikio yake, Hospitali ya Apollo ya Indraprastha imejijengea historia kubwa katika ulimwengu wa tiba kwa kuwa hospitali ya kwanza nchini India kutibu wagonjwa 200 kutoka nchi hiyo moja.
Kwa mafanikio ya zaidi ya asilimia 90% upandikizaji wa Ini zaidi ya 500 umefanyika.
Hospitali za Apollo hufanya zaidi ya upandikizaji 537 wa ini, figo na moyo katika siku 238 na kufanya hospitali hiyo kuwa ya pili duniani katika kufanya upandikizaji wa idadi kubwa kwa kipindi kifupi.
Chini ya miaka mitatu tangu kuanzishwa kwake, timu katika Idara ya ugonjwa wa ini na upandikizaji ya hospitali ya Apollo, imefanya upandikizaji wa ini zaidi ya 100 Juni 2011, na hivyo kujichukulia umaarufu mkubwa Chennai.
Upandikizaji wa ini wa mafanikio kwa watoto na watu wazima kwa mara ya kwanza ulifanywa katika Hospitali ya Apollo ya Indraprastha, New Delhi mwaka 1998. Tangu wakati huo, kumekuwa hakuna kuangalia nyuma, na leo ni hospitali kubwa inayoongoza katika upandikizajia wa ini Asia ya Kusini. Baadhi ya mafanikio ya kihistoria yake ni:
• Upandikizaji wa mara ya kwanza wa ini kwa watoto -1998
• Upandikizaji wa mara ya kwanza wa ini kutoka kwa mtu aliyekufa -1998
• Upandikizaji wa mara ya kwanza wa ini na figo -1999
• Upandikizaji wa mara ya kwanza wa ini kwa watoto kutoka kwa mfadhili aliye hai -1999
• Upandikizaji wa mara ya kwanza wa ini kwa mtu aliyekwisha pandikizwa tayari -2002
• Upandikizaji wa mara ya Kwanza wa ini kwa mtoto kutoka kwa mtu aliyekufa -2007
• Upandikizaji mdogo wa ini kufanyika nchini India -2008
• Upandikizaji wa Ini na figo zaidi ya 250 ndani ya mwaka ulifanyika 2009.
• Timu ya Upandikizaji wa Ini katika Hospitali ya Apollo, Chennai imefanya upandikizaji wa Ini zaidi ya 200. Na hivi sasa ni ya tatu kwa ukubwa nchini India.