Mgeni rasmi katika shindano la Redd’s Miss Kigamboni 2013 Mbunge wa jimbo la Kigamboni Mh. Dr. Faustine Ndugulile (CCM) akiwa ameambatana na Meneja Masoko Taifa wa shirika la ndege la Precision Air Bw. Ibrahim Bukenya wakiwasili ukumbini.(Picha zote na Zainul Mzige wa Dewjiblog).
Mgeni rasmi katika shindano la Redd’s Miss Kigamboni 2013 Mbunge wa jimbo la Kigamboni Mh. Dr. Faustine Ndugulile (CCM) akisalimiana na Aliyewahi kuwa Miss Tanzania 1999 Hoyce Temu (Somo wa washiriki wa Redd’s Miss Kigamboni 2013). Kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Miss Tanzania, Bw. Prashant Patel.
Mgeni rasmi katika shindano la Redd’s Miss Kigamboni 2013 Mbunge wa jimbo la Kigamboni Mh. Dr. Faustine Ndugulile (CCM) akisalimiana na Mwenyekiti wa Kamati ya Miss Tanzania, Bw. Prashant Patel mara baada ya kuwasili ukumbini.
Meza ya Majaji ikiongozwa na Chief Judge Mwandaaji wa Miss Temeke Bw. Benny Kisaka (wa pili kushoto), Mkurugenzi wa CXC Tours and Safari Bw. Charles Hamka ( wa pili kulia), Mratibu wa Miss Ilala Juma Mabakila (Kushoto) na Mkuu wa Radio France nchini Bw. Victor Willy (kulia).
Mwandaaji wa mashindo ya Redd’s Miss Kigamboni 2013 Angella Msangi akiteta jambo na Chief Judge wa mashindano hayo.
Picha juu na chini ni Washiriki 11 wa Redd’s Miss Kigamboni wakifungua shindano hilo kwa show ya aina yake.
Wanenguaji wa Bendi ya FM ACADEMIA maarufu kama Wazee wa Ngwasuma wakitoa burudani wakati wa shindano la kumsaka Redd’s Miss Kigamboni 2013 lililofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye ukumbi wa Navy Beach Kigamboni jijini Dar.
Pichani juu na chini washiriki wa Redd’s Miss Kigamboni wakipita jukwaani mavazi ya ubunifu.
Washiriki wa Redd’s Miss Kigamboni 2013 ndani ya Beach Wear.
Mmoja wa majaji ambaye pia ni Mkurugenzi wa CXC Tours and Safari Bw. Charles Hamka akitangaza majina ya warembo waliofanikiwa kutinga tano bora.
Washiriki wa Redd’s Miss Kigamboni waliofanikiwa kutinga tano bora.
Aliyewahi kushika taji la Miss Tanzania 1999 Hoyce Temu ambaye pia ni Somo wa washiriki wa Redd’s Miss Kigamboni 2013 akiwauliza maswali washiriki waliofanikiwa kutinga tano bora kwenye shindano hilo.
Washiriki wa Redd’s Miss Kigamboni 2013 wakijibu maswali.
Wadau wa tasnia ya urembo wakishangilia baadhi ya washiriki waliokuwa wakijibu maswali yao bila kutetereka.
Miss Kigamboni 2012 Edda Slyvester anayemaliza muda wake akisubiri kukabidhi taji kwa Redd’s Miss KIgamboni 2013.
Miss Kigamboni 2012 Edda Slyvester aliyemaliza muda wake akimvisha taji mshindi wa shindano la Redd’s Miss Kigamboni 2013 Magdalena Olotu (aliyeketi) wakati wa shindano hilo lililofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye ukumbi wa Navy Beach Kigamboni jijini Dar.
Mshindi wa Redd’s Miss Kigamboni 2013 Magdalena Olotu (katikati) akila pozi katika picha ya ukumbusho na mshindi wa pili Latifa Mohamed (wa pili kushoto) na Mshindi wa tatu Irene Rajab ( wa pili kulia) pamoja na mshindi wa nne na wa tano.
Mgeni rasmi katika shindano la Redd’s Miss Kigamboni 2013 Mbunge wa jimbo la Kigamboni Mh. Dr. Faustine Ndugulile (CCM) akitoa nasaha zake kwa mshindi wa taji la Redd’s Miss Kigamboni 2013 Magdalena Olotu mara baada ya kuibuka kidedea wa taji hilo ambapo amemtakia Baraka zote kuiwakilisha vyema Kigamboni.
Mgeni rasmi katika shindano la Redd’s Miss Kigamboni 2013 Mbunge wa jimbo la Kigamboni Mh. Dr. Faustine Ndugulile (CCM) akimkabidhi zawadi ya fedha taslimu shilingi 500,000/mshindi wa taji la Redd’s Miss Kigamboni 2013 Magdalena Olotu iliyotoka mfukoni kwa Mbunge huyo.
Meneja Masoko Taifa wa shirika la ndege la Precision Air Bw. Ibrahim Bukenya akikabidhi zawadi ya fedha taslimu shilingi 250,000/ kwa mshindi wa tatu wa Redd’s Miss Kigamboni 2013 Irene Rajab.
Mwenyekiti wa Kamati ya Miss Tanzania, Bw. Prashant Patel katika pozi na mshindi wa pili wa shindano la Redd’s Miss Kigamboni 2013 Latifa Mohamed mara baada ya kumkabidhi zawadi ya fedha taslim shilingi 300,000/.
Redd’s Miss Kigamboni 2013 Magdalena Olotu katika pozi na kitita chake cha fedha taslim shilingi 500,000/ zilizotolewa na Mbunge wa Jimbo la Kigamboni Mh. Dr. Faustine Ndugulile
Raia wa kigeni kutoka China aliyehudhuria shindano la Redd’s Miss Kigamboni 2013 akichukua picha ya ukumbusho ya mshindi wa taji hilo.
Mwandaaji wa shindano la Redd’s Miss Kigamboni 2013 Angella Msangi (kulia) na Mratibu wa shindano hilo, Somoe Ng’itu pamoja na Meneja Masoko Taifa wa shirika la ndege la Precision Air Bw. Ibrahim Bukenya (kushoto) wakati wa zoezi la kukabidhi zawadi kwa washindi.
Raia wa Kigeni kutoka china ndani Redd’s Miss Kigamboni 2013.
VIP Table… Alikuwepo Bw. William Malecela a.k.a LEMUTUZ, Katibu Mkuu wa kamati ya Miss Tanzania, Bw. Bosco Majaliwa, Aliyewahi kuwa Miss Tanzania 1999 Hoyce Temu (Somo wa washiriki wa Redd’s Miss Kigamboni 2013), Mwenyekiti wa Kamati ya Miss Tanzania, Bw. Prashant Patel wakati wa shindano la kumtafuta Redd’s Miss Kigamboni lililofanyika usiku wa kuamkia leo katika ukumbi wa Navy Beach Kigamboni.
Picha juu na chini ni baadhi ya Wadau wa tasnia ya masuala ya Urembo kutoka sehemu mbalimbali za jiji la Dar waliohudhuria shindano la Redd’s Miss Kigamboni 2013.
Nyomi ya Ukweli… Clouds Tv walikuwepo kuhakikisha shindao hilo linaruka Live.
Aliyewahi kushika taji la Miss Tanzania 1999 Hoyce Temu ambaye pia ni Somo wa washiriki wa Redd’s Miss Kigamboni 2013 akifurahi jambo na baadhi ya wageni waalikwa.