Magaidi Yahofiwa Kushambulia Michuano ya Euro 2016

Summer European Championship

Summer European Championship

TAIFA la Marekani linahofia kwamba huenda michuano ya soka ya Euro 2016 itakayofanyika nchini Ufaransa mwezi ujao ikashambuliwa na magaidi.

Idara ya masuala ya kigeni nchini Marekani imesema idadi kubwa ya watalii wanaotembelea Ulaya katika miezi ya kiangazi huenda pia ikawavutia washambuliji hao hivyo kutoa tahadhari.

Michuano ya Euro 2016 inatarajiwa kuandaliwa kuanzia Juni 10 hadi Julai 12, 2016 katika maeneo tofauti. Tayari taifa la Ufaransa limewekwa katika hali ya tahadhari kufuatia shambulio la Islamic State lililofanywa mjini Paris.

Katika tahadhari yake ya kusafiri iliotolewa kwa raia wake, wizara hiyo imeonya kuhusu hatari ya mashambulio ya wapiganaji hao barani Ulaya.

Taarifa zinabainisha kuwa mashambulio hayo yanaweza kulenga maeneo ya kitalii, migahawa, vituo vya biashara na vituo vya usafirishaji.
-BBC