Mafuriko Yavamia Tamasha Ujerumani, Wasanii Waponea Chupu Chupu

Maji yakivamia eneo la tamasha

Mafuriko Yavamia Tamasha Ujerumani, Wasanii Waponea Chupu Chupu



JUMAMOSI
ya Juni Mosi 2013, katika viwanja vya maonesho ya Wurzburg Festival, ilikuwa ni majonzi na simanzi baada ya eneo hilo kukumbwa na mafuriko yalisababisha hasara kubwa na kuvunjwa kwa tamasha hilo lililokuwa likisherekea maadhimisho ya miaka 25.

Habari za uhakika zimevuja kuwa vikosi vya zimamoto na wanausalama viliingiwa na mashaka baada ya wasanii wa Ngoma Africa Band a.k.a FFU, kutoweka ghafla katika chumba cha kubadilishia nguo (back Stage) na kutojulikana waliko. Wasiwasi ulitanda zaidi baada ya watu kuhisi watakuwa wamezolewa na mafuriko!

Hata hivyo hofu iliondoka baada ya saa kadhaa ambapo watayarishaji waligundua kuwa mkuu wa bendi hiyo field-marshal Kamanda Ras Makunja alikiondoa kikosi chake baada ya makachero wa bendi hiyo maarufu kama “Anunnaki Empire” kumtonya boss wao kuwa eneo la festival sio salama.

Mto ulio jirani na eneo hilo ulijaa maji kablda ya kadhia hiyo, hivyo Kamanda bila kuaga alikiondoa kikosi cha FFU wa Ngoma Africa katika hali ya usiri na kuwanusuru vijana wake na kuzima simu hadi baada ya saa fulani ndipo ikawashwa na kuwajulisha waandalizi wa onesho wasiwe na shaka kamanda na kikosi cha Ngoma Africawapo salama kambini, kitendo hiko kiliwaacha midomo wazi baadhi ya wadau! Wengine kudiriki kusema kuwa ‘Simba ni Simba’.

Tamasha hilo lilianza Mai 31, 2013 kukiwa na maelfu ya watu na wasanii mbali mbali walioalikwa wakiwamo mkongwe Manu Dibando, Alfa Blondy, Salifu Keita ndio walioanza kufungua dimba, Ijumaa hiyo hali ilikuwa shwari lakini ilipofika jumamosi hali ya hewa ilianza kubadilika kwa mvua na upepo,wasinii wengine wakiwa kwenye vyumba vya kujitayarishia miongoni mwao wakiwamo “Ngoma Africa band ” a.k.a FFU Ughaibuni, baada ya hali ya hewa kuanza kubadilika kwa upepo na mvua ndio.

inasemekana kuwa Kamanda Ras Makunja na kikosi chake Ngoma Africa band, Kuondoka katika eneo la festival (eneo la hatari) lilikumbwa na maji, katika mazingira ya ajabu. Watonyaji wa habari wamedai kuwa walitoroshwa kwa magari mawili meusi aina ya van yalikuwa na madilisha ya kiza.Kamanda Ras Makunja kateleza kama nyoka na kikosi chake. Mafuliko hayo yamevamia pia baadhi ya miji nchini Ujerumani na ulaya ya mashariki ka kusababisha vifo vya watu 12.