Maendeleo ya Jamii Waelezea Mikakati…!

Mkurugenzi wa Kitengo cha Mashirika yasiyo ya Kiserikali (NGO’s) wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, Marcel Katemba akiongea na waandishi wa habari (Hawapo pichani) kuhusu juhudi zinazofanywa na serikali katika kuyajengea mazingira mazuri ya ufanyaji kazi Mashirika yasiyo ya Kiserikali (NGO’s) ili kuongeza ushiriki na kutoa mchango wao katika kuleta maendeleo katika jamii, Wakati wa Mkutano uliofanyika jiijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Wizara hiyo Bw. Erasto Ching’oro. PICHA NA GEORGINA MISAMA.

Na Jovina Bujulu – MAELEZO

SERIKALI kupitia uratibu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto imeendelea kujenga mazingira wezeshi kwa ajili ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGO’s) kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya ya jamii.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa usajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Marcel Katemba leo jijini Dar es Salaam. Mercel alisema kuwa serikali inaendeleza jitihada za kuwezesha Mashirika hayo ikiwemo utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ya mwaka 2001 na Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Na.24 ya mwaka 2002 na marekebisho yake ya mwaka 2005.

“Sera hii ni mwongozo mkuu kwa Taifa katika masuala ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ikiwa na lengo la kuweka mazingira wezeshi kwa Mashirika hayo kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya jamii kwa kuzingatia uwazi, uwajibikaji na ushirikano,” alisema Marcel.

Marcel aliongeza kuwa Bodi ya Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali inaendelea kusimamia sekta ya mashirika hayo na kutoa ushauri kwa Waziri mwenye dhamana ya uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ili kuongeza ufanisi katika usimamizi wa sekta hiyo.

Aidha Baraza la Taifa la NGO’s linaendelea kuratibu utekelezaji wa kanuni za maadili ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kwa lengo la kujitawala, kutandaa na kuboresha huduma zinazotolewa na mashirika hayo.

Akifafanua zaidi Marcel amesema ubia na ushirikiano baina ya Serikali na NGO’s umeimarika kutokana na matamko ya kisera na elimu inayotolewa kwa wadau mbalimbali wa mashirika yasiyo yakiserikali.
Pia Serikali imeendelea kutoa misamaha ya Kodi na ruzuku kwa Mashirika hayo ikiwa ni sehemu ya kuthamini mchango wao katika maendeleo ya Taifa.

Juhudi za serikali za kujenga mazingira wezeshi kwa NGO’s zimepanua wigo kwa wananchi kujumuika na kushiriki katika maendeleo ya jamii ambapo zaidi ya wananchi 35,000 ni wanachama wa mashirika hayo yaliyo zaidi ya 6679 kote nchini.