Madiwani Rombo Waomba Shule za Walemavu, DC Alia na Ukame..!

Moja ya Shule za Wilayani, Rombo.

Moja ya Shule za Wilayani, Rombo.


Yohane Gervas, Rombo

MADIWANI wa Halmashauri ya Wilaya ya Rombo, wamesema ipo haja ya halmashauri hiyo kuongeza idadi ya shule za walemavu kwani shule mbili zilizopo kwa sasa hazitoshi. Aidha wameitaka halmashauri hiyo kuboresha miundombinu ya shule za walemavu zilizopo katika wilaya ya rombo ikiwemo barabara na vifaa vya kufundishia pamoja na kuongeza waalimu wa wanafunzi wenye uhitaji.

Akijibu hoja za madiwani hao kwa niaba ya mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Rombo Anthoni Tesha, Mwenyekiti wa kamati ya Elimu Afya Na maji, Abdalah Mbaga amesema kuwa halmashauri hiyo inafanya sensa ya walemavu kwanza ili kouna kama kuna haja ya kujenga shule mpya.

Aidha mbaga aliongeza kuwa pia halmashauri hiyo imejipanga kuweka vitengo vya walemavu katika shule zote zilizokaribu ili walemavu waweze kupata haki yao ya msingi karibu na maeneo yao wanayoishi. Serikali ya wilaya ya Rombo koani kilimanjaro imesema kuwa itaendelea kuhamasisha wananchi juu umuhimu wa utunzaji wa mazingira.

Wakati huo huo, Mkuu wa wilaya ya Rombo Elinas Pallengyo ameyasema hayo hivi karibuni wakati alipokuwa akizungumza katika kikao cha baraza la madiwani. Amesema kuwa wilaya hiyo inaweza kukumbwa na ukame endapo wananchi watazidi kuharibu mazingira kwa kukata miti kiholela katika maeneo yao na katika vyanzo vya maji.

Amesema kuwa wanaendelea kuwahamasisha wananchi kupanda miti kwa wingi katika maeneo wanayoishi sambamba na kuwakamata wananchi wote wanaokata miti kiholela. Aidha amewataka madiwani wa halmashauri hiyo pamoja na watendaji wa vijiji kushirikiana na serikali katika suala hilo la kuwahamasisha wananchi juu ya umuhimu wa utunzaj wa mazingira.

Na katika hatua nyingine mkuu huyo wa wilaya amesema kuwa wilaya hiyo itaendele kupambana na kuzuia unywaji wa pombe wakati wa kazi pamoja na unywaji na uuzaji wa pombe haramu ya Gongo katika wilaya Rombo.