Madereva Wetu Ndio Husababisha Misongamano Isiyo ya Lazima Barabarani!

20140501-093838.jpg

20140501-093855.jpg

20140501-093914.jpg

20140501-093932.jpg
Picha zinaonyesha magari (mara nyingi Daladala) yakiendeshwa upande wa gari zitokazo upande wa pili, maarufu kama “Kutanua”! Tabia hii imekuwa ikisababisha misongamano, isiyokuwa ya lazima kwenye barabara zetu za Dar.

Nidhamu ya matumizi ya barabara imetoweka kabisa Tanzania, sijui tunaelekea wapi? Ajali zinachukua maisha ya watu na mali Kila kukicha. Picha hizo zimenaswa kwenye barabara itokayo Tandika kwenda Buza, maeneo ya relini.

Picha na Mpigapicha Wetu Maalum, Dar.