
Mwenyekiti mpya wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan Madabida, akizungumza baada ya kutangazwa mshindi katika uchaguzi uliofanyika jana Oktoba 13, 2012 kwenye ukumbi wa PTA, jijini.

Wagombea wa Nafasi ya Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, kutoka (kushoto) ni Ramadhan Madabida, Chizii na Guninita, kabla ya kuanza kwa mchakato wa uchaguzi.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiteta jambo na Mwenyekiti mpya wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan Madabida, baada ya Mwenyekiti huyo kutangazwa rasmi kushika nafasi hiyo kwa kumshinda mpinzani wake, J. Guninita kwa kura 310 kwa 214, katika uchaguzi uliofanyika jana Oktoba 13, kwenye ukumbi wa PTA jijini Dar es Salaam. Picha na OMR