Mada Maugo na Kalama Nyilawila Kuzipiga Machi 8

Mada Maugo kushoto na Kalama Nyilawila wakitunishiana misuli wakati wa utambulisho wa mpambano wao utakaofanyika March 8 katika ukumbi wa P.T.A Sabasaba

Mada Maugo kushoto na Kalama Nyilawila wakitunishiana misuli wakati wa utambulisho wa mpambano wao utakaofanyika March 8 katika ukumbi wa P.T.A Sabasaba

Katibu mkuu wa chama cha ngumi za kulipwa nchini Antoni Rutta katikati akiwainua mikono juu mabondia Mada Maugo na Kalama Nyilawila wakati wa utambulisho wa mpambano wao utakaofanyika march 8 katika ukumbi wa P.T.A Sabasaba Picha na Super D Blog.

MABONDIA wenye upinzania mkali Mabondia Mada Maugo pamoja na Kalama Nyilawila wanatarajia kupanda jukwaani kuzipiga ili kumaliza ubishi. Pambano hilo linatarajia kufanyika Machi 8, 2015 katika Ukumbi wa P.T.A Sabasaba jijini Dar es Salaam.

Wakati huo huo mabondia wenye uzito wa juu nchini Aliphonce Mchumiatumbo na Iddi Kipandu ‘Iddi Bonge’ watapambana Feb 14 katika ukumbi wa P.T.A sabasaba wakigombania ubingwa wa taifa pamoja na pikipiki akizungumzia mpambano huo promota Shabani Manyoka amesema kupitia kampuni ya Mahamba Incorporation Limited wameamua kuandaa mpambano huo wa uzito wa juu ambao ni adimu sana nchini kufanyika na ndio unaokubalika duniani kote.

Mpambano huo wa raundi kumi utakuwa ni wa aina yake kwa kuwa kutakuwa na mapambano mengine ya utangulizi ambapo bondia Iddi Mnyeke atapambana na Yonas Sego wakati Sahani Kaoneka atamkabili Saidi Mbelwa, na Deo Samweli akipambana na Adam Ngange Juma fundi atakabiliana na Bakari Ostadhi na Amani Bariki ‘Manny Chuga’ atapambana na Mohamed Kashinde siku hiyo pia kutakuwa na mpambano mwingine wa utangulizi wa uzito wa juu kati ya Bank Mwakalebela atakae mkabili Frank Kimbwilo

Manyoka aliongeza kwa kusema kuwa siku hiyo kutakuwa na ulinzi wa kutosha ndani na nje ya ukumbi huo ambapo amesha wasiliana na walinzi mbalimbali.