BONDIA Francis Miyeyusho amewaongoza mabondia wa Tanzania katika zoezi l upimaji afya dhidi ya pambano lake dhidi ya bondia Fidelis Lipupa kutoka Zambia mchezo ambao ni pambano la kirafiki la kimataifa, linalotarajiwa kupigwa kesho katika ukumbi wa Dar Live jijini Dar es Salaam.
Zoezi zima la upimaji liliongozwa na Katibu Mkuu wa ngumi za kulipwa Ibrahim Kamwe akisaidiwa na Dk. Madono. Mabondia karibu wote waliopima wapo vizuri kwa mapambano yao wakati Francis Miyeyusho amekutwa na kilo 55.5 huku mpinzani wake Fidelis Lipupa akiwa na kilo 56. Ramadhan Kido wa Dar es Salaam amekutwa na kilo 89.7 na mpinzani wake kilo 90.2. Pia kutakuwepo na mapambano mengine manne ya utangulizi na mabondia waliopima wamewiana vema katika vipimo vyao wakiwemo dada Esther na Lulu.