Na Mwandishi Wetu
KOCHA wa Kimataifa wa mchezo wa Masumbwi nchini anaefundisha Timu ya Ashanti pamoja na timu ya Mkoa wa Ilala Kimichezo Rajabu Mhamila ‘Super D’ amevutiwa na mashabiki wa mchezo huo Mkoa wa Pwani.
Baada ya kuvutiwa na umati mkubwa uliojitokeza katika mpambano uliofanyika Bagamoyo mkoani wa Pwani mwishoni mwa wiki iliyopita mpambano uliofanyika katika Ukumbi wa Saadan High Way ambapo ulihudhuriwa na idadi kubwa ya mashabiki wa Bagamoyo.
Mpambano huo ulioandaliwa na Sharif Muhsin na kuratibiwa na bondia wa siku nyingi Said Yazidu umefungua ukurasa mpya kwa wakazi wa Bagamoyo kuukubali mchezo huo na kuendelea kuupenda na kuwapa sapoti mabondia wanaowakilisha Bagamoyo.
Baadhi ya mabondia waliopigana katika mpambano huo ni Maneno Zele aliyepata kichapo kutoka kwa bondia Baisa Juma wakati Zumbe Kikuru alimtwanga kwa K’O Tomo Kato katika raundi ya kwanza huku Kadani Rhamwana akimshinda Ndumbo Hassani kwa point. Mpambano huo ni wa pili kufanyika kwa mwaka huu umendelea kuwa chachu ya kupata vipaji vipya vya mchezo wa ngumi hapa nchini