KATIBU Kata wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mwananyamala, Rehema Mbegu ameahidi kutoa baskeli kwa Mabondia wa Klabu ya Mazoezi ya Bigright ya Mwananyamala Dar es Salaam.
Kiongozi huyo wa vijana ambaye amekuwa karibu na vijana wa klabu hiyo ikiwa ni pamoja kuwasaidia kwa chakula na utoaji ushauri, amesema msaada huo wa baiskeli utawasaidie kuzitumia kwenda shuleni na mazoezini.
Mbali na hayo Mbegu amesema ameamua kutoa baiskeli ili kuhamasisha ushindani zaidi na kuwapa moyo vijana kupenda zaidi michezo kuliko vijiwe.
Baada ya kuhakikishiwa kuwa kila bondia atakae shinda toka klabu ya
ngumi ya bigright atazawadiwa baskeli, wameahidi kukatika mikono
ulingoni yaani ni lazima washinde na wamebadilisha mfumo mzima wa
mazoezi, kwa sasa wapo pamoja, kikambi zaidi nyumbani kwa kocha wao
Ibrahim Bigright na kuongeza muda zaidi wa mazoezi kwa sasa wanafanya
mara tatu hadi nne kwa siku.
Mabondia hao ambao wanategemea kupanda ulingoni Julai 15 DDC-Kariakoo
ni Issa Omar (Bigright boxing) atakaechapana na Ramadhan Kumbele toka
kambi ya matumla katika uzani wa fly, Mwaite Juma toka bigright boxing
atapigana na mkongwe Anthony Mathias katika uzani wa bantam.
Ambao watakuwa wakisindikiza pambano la ubingwa wa taifa kati ya Juma
Fundi wa Keko na Baina Mazola wa Mabibo toka kambi ya mzazi. Mapambano hayo yameandaliwa na kaike siraju na kusimamiwa na TPBO