MIAMBA wawili wa mchezo wa ngumi wenye nywele zilizotengenezwa kwa mtindo wa rasta, ambayo mara nyingi huwa ndio gumzo la watu mitaani hususani wapenda mchezo wa ngumi kwa tabia zao na vibwekwa vyao kwa raia, yaani mabondia Japhet Kaseba na ‘Mtukutu’ Thomas Mashali Jumamosi ya Machi 29, 2014 katika ukumbi PTA viwanja vya maonesho Sabasaba wanatarajia kukutana.
Bondia Mashali ‘samba asiyefugika’ kama anavojiita alizaliwa Septemba 1989 na kukulia mitaa ya Manzese jijini Dar es Salaam, akiwa mtoto mtundu, mkorofi, mgomvimgovi na mpenda michezo kama ilivyo kwa mdogo wake Charles Mashali ambaye na yeye pia alikuwa bondia mzuri aliyetokea kuwashinda na kuwasumbua mabondia wengi kama kina Francis Miyeyusho na aliwahi kuchukua ubingwa wa taifa kabla ya kuachana na mchezo wa ngumi kwa kuumia bega ambalo linamfanya ashindwe kuendelea na mchezo huo.
Thomas Mashali ambae ni mkubwa kwa Charles Mashali alianza mchezo wa ngumi akiwa mdogo na kupigana mapambano katika kumbi za Colin na Manyala Park za Manzese na hapo udogoni amewahi kucheza na kina Ramadhan Miyeyusho, Raston Phili ‘moto wa tipa’ na marehemu Papa Upanga na kuwa kivutio cha wengi ulingoni.
Aprili 2012 Mashala alikutanishwa na Seleman Galile kugombania ubingwa wa taifa wa TPBO ambao alishinda mchezo huo kwa pointi na kuuchukua ubingwa huo kwa taabu sana katika pambano wa gumi, ubingwa ambao bado anaushikilia mpaka leo. Baadaye alifanikiwa kupambana kimataifa na kuwashinda mabondia wengi wa nje hususani Kenya na Uganda na kutwaa ubingwa wa Africa Mashariki na Kati kwa kumchapa Medy Sebyala wa Uganda.
Akiendeleza wimbi la ushindi Mashali “mzee wa ghetto au simba asiye fugika – kama anavyojiita” viongozi na wadau wa ngumi wakamkubali na kumuona ameivaa kimchezo wakaona huu ni muda muafaka wa Mashali kumvaa Francis Cheka akiwa anautaka ubingwa wa cheka, Mai 2013 akapoteza mchezo huo dhidi ya cheka ambao uliokuwa mkali baada ya kupigwa mwishoni wa raundi ya kumi.
Mashali alionesha upinzani mkali kwa cheka, akiwa anajiuliza kapigwaje na cheka alipata bahati nyingine ya kukutanishwa na bondia Mada Maugo kwa kugombea ubingwa wa Afika wa WBFed (world boxing federation) na kuibuka kidedea baada ya kumpiga Mada Maugo kwa pointi, na kutwaa ubingwa huo afrika akachaguliwa kwenda urusi kugombania ubingwa wa mabara dhidi ya arif magomedov huko alipata kipigo kikali toka kwa bondia huyo wa urusi katika raundi za mwazomwanzo na kurudi nchini mikono mitupu.
Japhet Kaseba aliyezaliwa Desemba 1979 ambaye ni bingwa hapa nchini kwa kukosa bondia wakupigana naye baada ya kuwapiga mabondia wote katika mchezo wa mateke (kickboxing) ambaye pia amewahi kuwa bingwa wa dunia katika mchezo huo wa ngumi na mateke (kickboxing) kwa kushinda ubingwa wa mabara nchini Holand na kuutetea nchini Japan, na baadaye kugombea ubingwa huo wa dunia dhidi ya bondia toka Ufilipino Ricky Agayas na kumpiga kwa KO ya raundi ya tatu na kutwaa ubingwa huo.
Kaseba amekaa kwa muda bila kupata nafasi ya kuutetea ubingwa wake huo kwa kukosa wadhamini na hapo alipoamua kubadili aina ya mapigano na kurudi katika ngumi mchezo ambao aliucheza zamani kabla ya kickboxing. Alipoingia tena katika ngumi alipata nafasi ya kupigana na bingwa wa ngumi Francis Cheka katika pambano la kuwakutanisha bingwa wa Mateke na bingwa wa ngumi matokeo yake Kaseba alishindwa na Cheka na kutoridhika na matokeo hayo kwa kisingizio cha fujo zilizotokea katika mchezo huo na akawa anatafuta marudiano kwa hali yoyote ile na kumfanya abakie katika ngumi akisubiri nafasi nyingine ya marudiano na Cheka. Kasema anashikilia Ubingwa wa taifa wa PST kwa kumpiga Maneno Osward.