BONDIA Fadhili Majia ambae ni Bingwa wa kimataifa wa UBO na Bingwa wa taifa wa flyweight-PST 2012, TPBO 2010, TPBC 2009 na chalenger wa ubingwa wa dunia wa WBO Afrika 2009 south Afrika amepima uzito na afya kiujumla kwa ajili ya kumkabili mpinzani wake NASIBU RAMADHANI ambae ni bingwa wa WBF (World Boxing Forum International Flyweight Title) 2011.
Zoezi zima la upimaji lilisimamiwa na TPBO likiongozwa na IBRAHIM
KAMWE na kusema ya kuwa mabondia wote wapo katika afya njema na uzani
wao wote wamepata 50.8kgs kwa pamoja hivyo wapo sawa kupigana kwa
mujibu wa sheria za ngumi.
Tukumbuke majia alikwishawahi kuwa bingwa wa ubingwa huu mwaka 2008 na
kuucha na kwenda kugombania ubingwa wa dunia south Afrika na hivyo
kukaa bila kuutetea na kuchukuliwa na Haji juma wa Tanga, kwa sasa upo
wazi na unagombewa tena na majia mwenyewe na nasibu Ramadhani bondia
chipukizi na asiyepigika karahisi.
Katika mpambano huo pia kutakuwa na mapambano ya utangulizi kama
ifuatavyo na uzani wao waliopimaleo katika mabano – Abdala
Mohamed” Prince Naseem” (63kgs) ataminyana na Seba Temba (64kgs) wa
Morogoro raundi6, Venas Mponji (58.5kgs) na Amos Mwamakula(60kgs),
Yohana Robert (62kgs) na Badi Mombasa (61), Kasim Mbundike (57kgs) na
Epson John wa Morogoro (57.8kgs), iddi Mnyeke 63 na Fadhili awadhi 63
mapambano yanategemewa kuanza saa kumi na moja jioni katika ukumbi wa
FRIENDS CORNER HOTEL