Mabadiliko Katika Upasuaji

Mabadiliko Katika Upasuaji

SEKTA ya afya duniani imeshuhudia mapinduzi yanayolenga kuongeza umri wa kuishi, ubora wa maisha, njia mbadala za uchunguzi, njia bora za matibabu, na pia ufanisi na ubora katika huduma za afya. Teknohama imekuwa na mchango mkubwa sana katika maendeleo ya ndani ya sekta hii muhimu. Makampuni yanayohusika na kutengeneza vifaa vya tiba hivi sasa yanalenga katika kutengeneza roboti ambazo hufanya upasuaji kwa ufanisi zaidi bila madhara makubwa kwa mgonjwa.

Kuna matumaini sana katika upasuaji kwa kutumia teknolojia ya Roboti. Teknolojia hii ni ishara ya mapinduzi katika sekta ya afya, na ni moja ya mambo muhimu yanayoongelewa sana katika upasuaji hivi leo. Mfumo wa upasuaji kwa kutumia roboti umeletwa ili kusaidia katika upasuaji mgumu, ambao hufanyika kwa shida, au unaohusisha maeneo ambayo ni magumu kufikika na hatari. Kwa kutumia mikono maalumu inayopatikana katika Roboti hilo upasuaji huo urahisishwa zaidi.

Mikono ya Roboti hudhibitiwa na kompyuta inayoendeshwa na mpasuaji kwa kutumia mikono na miguu. Hudhibiti huu ni sawa na ule wa mchezo wa video, maarufu kama ‘video game’ ambao huwezesha upatikanaji kwa usahihi zaidi wa maeneo magumu kufikika ikilinganishwa na njia iliyokuwa ikitumika awali ya ‘laparoscopic’.

Kutumia matundu madogo sana, upasuaji wa aina hii unaweza kuondoa uvimbe tata pasipo uharibifu wa tishu na pia humsaidia mgonjwa kutokaa hospitalini muda mrefu pamoja kupona ndani ya muda mfupi. Teknolojia hii inapunguza hatari ya uharibifu wa mishipa na tishu katika eneo husika.

Upasuaji kwa kutumia Roboti unaweza kutumika kutibu hali mbalimbali kama vile magonjwa ya kina mama (gynaecologic), ikiwa ni pamoja kuondoa mfuko wa uzazi (hysterectomy), kutibu maambukizi kwenye leya ya ndani katika mfuko wa uzazi (endometriosis), uvimbe kwenye mfuko wa uzazi (fibroids uterine), saratani ya shingo ya kizazi, saratani ya mfuko wa kizazi, fistula na viungo katika nyonga kutoka nje (pelvic organ prolapsed).

Utaratibu wa upasuaji na ushonaji unaweza kufanyika kwa usahihi zaidi kupitia teknolojia hii. Kulingana na huduma ya afya inayoitajika na umri wa mgonjwa, upasuaji kutumia Roboti pia unaweza kusaidia kuboresha afya ya uzazi na kumsaidia mgonjwa uwezo wa kuzaa.

Kwa wagonjwa wa Saratani, mara nyingi upasuaji wa aina hii huusisha upasuaji wa kichwa, shingo, ulimi, tezi dume, magonjwa ya wanawake, kuondoa uvimbe kwenye utumbo (colorectal surgery) na upasuaji unaohusisha nyonga.

Mfumo huu wa upasuaji una msaada mkubwa kwa wagonjwa ambao wanahitaji upasuaji wa tezi upasuaji unaohusisha kuchana sehemu ya chini ya shingo. Kwa kutumia roboti sasa inawezekana kufanya upasuaji wa tezi bila kuchana shingo kwa sehemu kubwa na bila kuacha kovu inayoonekana.

Mwaka 2012 Ashura Ibrahim, msichana mwenye umri wa miaka saba kutoka Tanzania alipewa nafasi nyingine katika maisha kupitia upasuaji kwa kutumia Robot. Mwaka 2010, mtoto huyo alipata ajali iliyohusisha Bajaji na gari mjini Dar-es-Salaam, janga hilo ilisababisha kuharibiwa kwa kibofu chake.

Pamoja na upasuaji kadhaa uliofanyika nchini, matokeo hayakuridhisha. Kwa msaada kutoka Wizara ya Afya na usitawi wa jamii, Ashura alipelekwa hospitali ya watoto ya Apollo mwaka 2011, ambapo alifanyiwa upasuaji kuimarisha kibofu cha mkojo.

Hata hivyo, akarudi baada ya mwaka, madaktari wakagundua kwamba akiwa katika hatua za uponyaji, mrija wa mkojo wa upande wa kushoto ulikuwa umeshuka chini isivyo kawaida, na kusababisha mkojo kurudi kwenye figo. Hii ingeweza kusababisha uharibifu wa figo au maambukizi yanayosababishwa na mkojo.

Dk. Sripathi alisema kwamba upasuaji wa kawaida usingeweza kufanyika, kwa vile alikuwa tayari amefanyiwa upasuaji mara kadhaa. Ilibid afanyiwe upasuaji aina ya ‘Laparoscopic’, lakini huu pia haukuweza kufanyika kwa sababu kufanya kazi kwa kutumia vyombo viwili vigumu ilikuwa sio vizuri kiutaratibu, hivyo chaguo la mwisho ilikuwa kutumika kwa Da Vinci robot. Upasuaji uliochukua muda wa masaa matatu kwa kutumia mikono maalumu ya robot, na bila kupasua upya kibofu cha mkojo, mirija hiyo iliweza kurudishwa sehemu yake ya kawaida.

Upasuaji huo ulimuacha mtoto Ashura na majeraha madogo sana kwenye tumbo lake. Dr Sripathi aliongeza kuwa upasuaji huu ni wa kwanza ukihusisha kibofu cha mkojo, na kwamba tatizo hilo limeondolewa siku moja tu na hakuna damu iliyokuwa ikionekana katika mkojo baada ya upasuaji.

Dk. Rooma Sinha, Mshauri Mwandamizi wa magonjwa ya wanawake, na upasuaji katika hospitali ya Apollo; Hyderabad nchini India, ameelezea faida ya upasuaji kwa kutumia Roboti. Anasema kuwa, “teknolojia ya kutumia Robot katika upasuaji itadumu sana kama tunaweza kuona faida nyingi za teknolojia hii ikilinganishwa na njia mbalimbali za zamani za upasuaji. Ni hatua ya pili ya upasuaji kwa kutumia mashine maalumu huku ukiangalia kwenye Skrini ya computer (laparoscopic). Hii itapunguza haja ya kufanya upasuaji wa wazi kwa wagonjwa wenye matatizo ya uzazi “.

Anaongeza kuwa, “Upasuaji wa kutumia Robot ni njia mpya ya upasuaji ya isiyo na madhara na inajumuisha upasuaji wa kawaida (Open surgery) na Upasuaji wa kutumia skrini ya computer (laparoscopic). Kwa msaada wa Mikono maalumu ya Robot inayodhibitiwa, daktari anaweza kufanya upasuaji kupitia mikato midogo sana. Teknolojia hii husababisha kutokuwa na makovu makubwa yatokanayo na kukatwa sana, kutokuwepo na upungufu wa damu, maumivu baada ya upasuaji na kupona kwa haraka zaidi “.

Mwaka jana, Hospitali Apollo mjini Hyderabad imefanikiwa kufanya upasuaji mfululizo wa tezi kupitia teknolojia hii. Hakuna shaka kwamba upasuaji wa kutumia Robot ni kiungo muhimu katika masuala ya upasuaji, mchango huu muhimu unajidhihirisha hata katika nchi zinazoendelea.

Kuhusu Hospitali ya Apollo
Hospitali za Apollo ni za kwanza katika eneo Asia Pacific kutoa huduma za upasuaji kwa kutumia mfumo huu wa Robot, ambayo ni aina ya upasuaji isiyokuwa na madhara. Taasisi ya upasuaji kutumia Robot iliyopo hospitalini hapo wamejitoa kipekee katika kutoa huduma bora kwa wagonjwa.

Taasisi ina wataalamu waliobobea kwenye mafunzo ya upasuaji, upendo katika utoaji wa huduma vifaa vya matibabu vya kisasa vinavyolenga kutoa uzoefu bora kwa mgonjwa. Vifaa hivyo ni pamoja na vifaa Robot ya Da Vinci inayotumika katika upasuaji.

Mfumo huu wa upasuaji hutumika katika teknolojia ya upasuaji wa magonjwa yanayohusiana na mfumo wa mkojo (Urology), magonjwa ya wanawake (Gynaecology), moyo, utumbo, na magonjwa ya watoto na matatizo ya uti wa mgongo.