Maandalizi Uzinduzi Jengo la Kijitonyama Lutheran Centre

Baadhi ya wajumbe wa kamati ya maandalizi ya uzinduzi wa Jengo la Kijitonyama Lutheran Centre(KLC)kama linavyoonekana pichani litakalozinduliwa Aprili 29, Jengo hili litatumika kama kitega uchumi wa KKKT-Dayosisi ya Mashariki ya Pwani.

Katibu wa baraza la kanisa hilo Dk. Victoria Kayombe akiongea na baadhi ya wanakamati ya maandalizi ya uzinduzi wa jengo la Kijitonyama Lutheran Centre (KLC)litakalotumika kama Kitega Uchumi wa Kanisa hilo, mara baada ya kumaliza mkutano na waandishi wa habari juu ya uzinduzi wa jengo hilo utakaofanyika Jumapili ya tarehe 29 mwezi huu, wa pili kutoka kushoto Mchunga wa Usharika wa Kijitonyama Ernest Kadiva, Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya uzinduzi Selina Mkony, Mzee wa baraza la kanisa Leonard Shayo na Mjumbe wa kamati hiyo Peniel Uliwa. Ujenzi huo umegharimu kiasi cha bilioni 3.5.

Mchungaji wa usharika wa kijitonyama Ernest Kadiva akifafanua jambo kwa wanakamati ya maandalizi ya uzinduzi wa jengo la kitegauchumi cha usharika huo litakalojulikana kama KIJITONYAMA LUTHERAN CENTRE (KLC) litazinduliwa jumapili tarehe 29 mwezi huu,Ujenzi wa jengo hilo ulianza mwaka 2009 na kugharimu jumla ya sh. bilioni 3.5.