Maafisa wa Zimbabwe kuchunguzwa

Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe

Afrika Kusini ni sharti ichunguze maafisa wa Zimbabwe wanaodaiwa kuhusika na tuhuma za mateso dhidi ya wanasiasa wa upinzani mwaka 2007, kulingana na uamuzi wa mahakama kuu nchini Afrika Kusini.
Jaji wa mahakama hiyo amesema kuwa chini ya sheria za kimataifa Afrika kusini ina jukumu la kuchunguza tuhuma za ukiukwaji wa haki za kibinadamau.
Awali Viongozi wa mashtaka walikataa kuchunguza maafisa waliotuhumiwa na ambao walikuwa nchini humo kwa muda.
Afrika Kusini ilikuwa nchi ya kwanza barani Afrika kutambua mahakama ya kimataifa ya jinai.
Kesi hiyo ilifikishwa mbele ya mahakama na shirika la Southern Africa Litigation Centre (SALC), pamoja na shirika linalowakilisha raia wa Zimbabwe waliotorokea nchini humo, wengi ambao jamaa zao wako nchini humo baada ya kusema kuwa waliteswa na maafisa wa usalama wa Zimbabwe .
Kesi hii ilifikishwa mahakamani baada ya tukio moja mnamo mwaka 2007, ambapo wafuasi wa aliyekuwa kiongozi wa chama cha upinzani MDC kusema kuwa waliteswa baada ya msako dhidi ya makao makuu ya chama

-BBC