MAOFISA polisi watatu wametiwa gerezani baada ya kukutwa na hatia ya kuhusika kwenye mauaji ya mwanafunzi kutoka Burkina Faso mwezi Februari, na kuchochea ghasia kwa wiki kadhaa. Justin Zongo alifariki dunia baada ya kudhalilishwa akiwa mikononi mwa polisi. Awali serikali ilisema kifo chake kilisababishwa na homa ya manjano, na kusababisha hasira miongoni mwa wengi.
Maandamano- yaliyozidi kupamba moto kutokana na kupanda kwa bei za vyakula- yalisambaa nchini kote, hata kusababisha uasi wa kijeshi. Ghasia hizo zilionekana kuwa tishio kubwa kwa uongozi wa Blaise Compaore uliodumu kwa miaka 24.
Rais Compaore aliifukuza serikali yake na kuwabadilisha wakuu wake wa usalama.
Maofisa hao wawili wa polisi walihukumiwa kifungo cha miaka 10 jela na miaka mengine minane kwa kuchochea wasaidizi wake wawili.
Wakili wa familia ya Bw Zongo alisema ni vyema kuwa “polisi wanajua wana wajibu wa kuheshimu haki za binadamu”, imeripoti shirika la habari la AFP. Lakini wakili wa polisi, Moumouny Kophia, alisema alikuwa ” na mshtuko mkubwa na mwenye kusikitishwa”. “Sihisi kwamba haki imetendeka.”
-BBC