Maadhimisho ya wiki ya Kifaransa Tanzania

International Organisation of Francophonie–OIF

‘Kifaransa- Lugha ya Umoja’

NCHI 13 zenye uwakilishi wa kidplomasia hapa Tanzania, zimeandaa kwa pamoja tamasha la utamaduni na michezo kwa ajili ya kuadhimisha wiki ya utamaduni wa Kifaransa tarehe 20 Machi hadi 31 Machi, 2012. Nchi 56 ambazo ni wanachama wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kifaransa (International Organisation of Francophonie–OIF) na 19 zenye uwakilishi wa utazamaji ambazo zinaongea Kifaransa duniani, zitasherehekea wiki hii kwa lengo la kukuza lugha ya Kifaransa chini ya msingi wa mshikamo wa lugha na tamaduni mbalimbali za kimataifa

Nchi wanachama wa OIF zenye ofisi za kibalozi Tanzania, ni Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ,Msumbiji, Ubelgiji, Vietnam; Kanada, Misri; Uswisi, Ufaransa, Burundi, Rwanda, Jibuti, Shelisheli na Komoro kwa pamoja zimeandaa tamasha la utamaduni na michezo kuadhimisha wiki ya utamaduni wa Kifaransa katika miji ya Arusha, Dar es Salaam na Zanzibar, kama ifuatavyo:

• Tarehe 20 Machi 2012- Ufunguzi wa maadhilisho utafanyika Forodhani- Kwenye Hoteli ya Slipway iliyoko Masaki Dar es Salaam. Ufunguzi rasmi atafanywa na Balozi wa DRC nchini, Mr. Juma Alfani Mapango na baadae bendi yenye asili ya Kongo; Junior Ringo Kalunde & Band itatumbuiza. Mgeni rasmi atakuwa Waziri wa Habari, Utamaduni; Utalii na Michezo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Ndugu Abdillahi Jihad Hassan

• Tarehe 23 Machi 2012 Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Mheshimiwa Marcel Escure, atamkaribisha Raisi wa Uchaguzi wa Kameruni Daktari Samuel Fonkam Azu kutoa mada juu ya malengo ya OIF katika kudumisha demokrasia, haki za kibinadamu na utawala wa sheria ili kuzua migogoro, namna ya kujinasua kutoka kwenye matatizo; mpito kuelekea demokrasia na kudumisha amani. Warsha hiyo itafanyika kwenye Asasi ya Kifaransa ya Dar es Salaam “ Alliance Française de Dar es Salaam”
.
• Tarahe 24 Machi 2012, Mwanamuziki mwenye kipaji na muimbaji kutoka nchi ya Ivori, Dobet Gnahore atacheza albamu yake mpya katika Ukumbu wa Utamaduni wa Kijerumani “ Goethe Institut” iliyopo Upanga; Atakuwa na kikundi chake cha wachezaji.

• Asasi ya Kifaransa ya Dar es Salaam (Alliance Française) imealika kikundi cha sanaa cha kuigiza cha Kifaransa “Cie Pied la Route” kuigiza tamthilia ya Mtunzi wa Kitabu cha hadithi kutoka Ivori, Ahmadou Kourouma “Mungu hakulazimika” (Allah n’est pas oblige). Kinahusu tamthilia ya wapiganaji- watoto na viongozi wa kivita katika nchi za Liberia na Sierra Leone katika miaka ya 90. Mchezo utachezwa kwa lugha ya Kifaransa na maandishi ya maelezo kwa iingereza.

• Mashindano ya ujuzi wa lugha ya Kifaransa yameandaliwa nchini kote kuanzia Mwezi Februari ambapo wanafunzi 1, 700 watashiriki. Sherehe ya kutoa tuzo kwa washindi wa mashindano hayo zitafanyika Allience Française tarehe 31 Machi 2012.

• Juhudi za kuanzishwa kwa Jumuiya ya Kimataifa ya Kifaransa zilianzishwa na wakuu watatu wa Nchi za Kiafrika mwaka 1970; ambao ni Leopold Senghor wa Senegali, Habib Bourguiba wa Tunisia, Hamad Dioro wa Niger na Mtoto wa Mfalme Sihanouk wa Kambodia. Nchi 21 wilikubaliana kutia saini mkataba wa kuanzisha ACCT ambapo mwaka 1988 Jumuiya ikabadilishwa kuitwa OIF. OIF ni Jumuiya ya jamiii inayounganishwa na lugha ya Kifaransa- katika Kifaransa “Ceux qui ont le Français en partage”. Jumuiya hii ina malengo ya kisiasa, kitamaduni na kiuchumi. Dira ya jumuiya hii iko katika malengo manne ambayo yamekubaliwa na wanachama wake:

 Kukuza lugha ya Kifaransa na uwiano wa Kitamaduni na lugha
 Kukuza amani, demokrasia na haki za binadamu
 Kusaidia sekta ya elimu, mafunzo, elimu ya juu na utafitii
 Maendeleo endelevu na mshikamano
Hivi sasa lugha ya Kifaransa, ni lugha ya kwanza au ya pili kwa zaidi ya watu millioni 200 duniani, nusu yao wakiwa wanaishi katika bara la Afrika na ni lugha rasmi ya mashirika mengi ya Kimataifa na yale ya Kikanda likiwamo Umoja wa Afrika
Katika Tanzania kumekuwa na ongezeko la watu wanaojifunza Kifaransa katika ngazi mbalimbali zikiwemo za kitaalamu.
Muamko huu ni jambo la kutia moyo kwa kuwa nchi hii inazungukwa na baadhi ya nchi jirani zinazoongea Kifaransa na ambazo zinajipanga kukuza utalii na zimeonyesha ari kubwa ya kujiunga na Jumuiya za Kiuchumi na Kisiasa za Kanda ya Afrika. Tujikumbushe kuwa nchi wanachama mbili ambazo ziko katika Jumuiya ya OIF Rwanda na Burundi zilijiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki Julai 1, 2007 .

Matokeo ya muamko huu ni kuanzishwa kwa programu ya miaka 3 ya kuwafunza waalimu wa Kifaransa ambayo imebuniwa na Serikali ya Ufaransa, Wizara ya Elimu na Mafunzo Ustadi, Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam na Chuo Kikuu Huria cha Tanzania ambayo inaendelea kutekelezwa.

Maadhimisho ya Kifaransa duniani, ni sherehe za kimataifa za kuendeleza tamaduni mbalimbali kupitia Kifaransa. Lugha ya Kifaransa ni daraja ambalo watu na nchi zenye tamaduni mbalimbali hupita kuelezea asili zao. Ni jukwaa la maelewano ambalo linaimarika kwa mahusiano na lugha na tamaduni nyingine kama: Kiingereza, Kiarabu, Kireno na Kihispaniola. Kifaransa ni lugha ya Kimataifa ambayo idadi ya wasemaji wake inakua kila kukicha. Na jukwaa hili lenye tamaduni mbalimbali zenye lengo la kuuunganisha dunia linaitwa : Ufungamano wa Tamaduni.