Mwanafunzi Hussein Hemed Hussein wa Shule ya Msingi Tusiime akipokea cheti cha pongezi
kwa kuwa mshindi Bora wa jumla katika mitihani ya Taifa kwa mwaka 2013 kwa shule za Binafsi za jiji
la Dar es salaam.
Mwanafunzi Joyce Lymo wa Shule ya Sekondari Kanosa, Kinondoni akionesha cheti cha
pongezi kwa kuwa mshindi Bora wa jumla kwa wasichana katika mitihani ya Taifa kwa mwaka 2013
alichokabidhiwa na Mkuu wa wilaya ya Ilala Bw. Raymond Mushi katika hafla ya Siku ya Elimu jijini Dar
es salaam.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Bw. Raymond Mushi akiongea na wadau mbalimbali wa elimu wa mkoa
wa Dar es salaam wakiwemo walimu wa shule za msingi na sekondari, wamiliki wa shule binafsi na
wanafunzi wakati wa hafla ya Siku ya Elimu mkoani Dar es salaam leo.Katika hafla hiyo washindi wa
mitihani ya taifa kwa mwaka 2013 kutoka shule za msingi na sekondari za serikali na binafsi
wametunukiwa vyeti na zawadi mbalimbali kutokana na ufanisi wao katika utekelezaji wa Mpango wa
Matokeo Makubwa Sasa (BRN).
Ofisa Elimu wa Mkoa wa Dar es salaam Bw.Raymond Mapunda akiongea na wadau mbalimbali wa
elimu wa mkoa wa Dar es salaam wakiwemo walimu wa shule za msingi na sekondari,wamiliki wa shule
binafsi na wanafunzi wakati wa hafla ya Siku ya Elimu mkoani Dar es salaam leo.
Wadau wa elimu wakiwemo wazazi, walimu wa shule za sekondari na msingi, wamiliki wa shule
binafsi na viongozi mbalimbali wakishangilia mafanikio na ushindi wa mkoa wa Dar es salaam katika
mitihani ya taifa ya shule za Msingi na Sekondari kwa mwaka 2013 leo jijini Dar es salaam wakati wa
hafla ya Siku ya Elimu. Picha zote na Aron Msigwa – MAELEZO.