Maadhimisho ya Siku ya Amani Duniani Jijini Dar es Salaam

Picha juu na Chini Wanafunzi wa shule mbalimbali za msingi na sekondari jijini Dar wakiwa wamebeba mfano wa Njiwa kuashiria Amani katika maadhimisho wakiandamana kuelekea ukumbi wa Karimjee katika maadhimisho hayo.

 

Maandamano barabarani.

Mgeni rasmi Dkt. Migiro (katikati), Dk. Kacou pamoja na Balozi wa Nigeria nchini Dk. Nanjabu (kushoto) wakiwa wamebeba sanamu mfano wa ndege aina ya Njiwa ikiwa ni Ishara ya Amani.

Mgeni rasmi Dk. Asha-Rose Migiro akiimba nyimbo za kuhamasisha amani pamoja na washiriki wa maandamano ya siku Amani Duniani.

Afisa Habari kutoka kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa Stella Vuzo akitoa utambulisho wa meza kuu.Katikati ni Mgeni rasmi Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Dk. Asha-Rose Migiro, Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa Dk. Alberic Kacou (wa pili kushoto), Mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la Right to Play Bw. Francis Rwiza (kulia), Balozi wa Nigeria nchini Tanzania Dk. Ishaya Nanjabu na Wa pili kulia ni Program Manager wa Global Network of Religions for Children (GNRC) Bi. Elizabeth Mwase.

Wanafunzi wa shule mbalimbali za jijini Dar wakati wa maadhimisho ya Siku ya Amani Duniani yenye Kauli mbiu “AMANI ENDELEVU KWA UENDELEVU WA MASIHA YA BAADAE”.

Mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya Amani Duniani aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Dkt. Asha-Rose Migiro akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Amani Duniani leo jijini Dar es Salaam, ambapo pamoja na mambo mengine amesema Tanzania itaendelea kuwa mfano wa jinsi demokrasi inavyofanya kazi katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Aidha amesema mchakato unaoendelea wa mabadiliko ya katiba umewaweka wanaume na wanawake wa Tanzania katika nafasi ya kuamua kuhusu kuimarisha manufaa ya Kidemokrasia, kuimarisha utawala bora na haki za binadamu.

Pichani ni baadhi ya mabalozi wanaowakilisha nchi zao pamoja na maafisa wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini wakisiliza hotuba ya mgeni rasmi Dk. Asha-Rose Migiro (hayupo pichani).

Baadhi ya wageni waalikwa wakiwamo wawakilishi kutoka Serikalini, Mabalozi na Viongozi kutoka Ofisi za Kibalozi na Wanafunzi kutoka shule mbalimbali za jijini Dar.

Mshindi wa Insha wa maadhimisho ya siku ya Amani Duniani kutoka Shule ya Sekondari Kibasila akisoma Insha yake mbele ya wageni waalikwa hawapo pichani.

Mkurugenzi wa shirika lisilo la Kiserikali la Right to Play Bw. Francis Rwiza akimkabidhi cheti pamoja na zawadi mshindi wa Insha ya maadhimisho ya siku ya Amani Duniani mwanafunzi wa shule ya msingi Airwing Brenda Simon.

Wanafunzi kutoka shule ya msingi Buguruni Viziwi wakitoa burudani wakati wa sherehe za maadhimisho hayo.

Dk. Asha-Rose Migiro akifanyiwa mahojiano na vyombo vya habari nchini.

Na Mwandishi Wetu

ALIYEKUWA Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Dk. Asha Rose Migiro amesema ili amani idumu nchini kuna ulazima wa raslimali za nchi zitumika kwa maendeleo. Migiro amesema amani iliyopo nchini ni ya kujivunia na inahitaji kutunzwa na kuheshimiwa.

Amesema hayo wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Amani duniani iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Dk. Migiro amesema ili amani idumu ni lazima iwepo mipango madhubuti ya kuhakikisha uchumi unakua kwa kila nchi na kuhakikisha kwamba raslimali za nchi zinatumika vizuri ili kuleta maendeleo.

Maadhimisho hayo yalihudhuriwa na mabalozi na baadhi ya viongozi wa serikali na wabunge.