Maadhimisho ya sala ya Iddi El Fitri Dar na Zanzibar

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa wakati alipowasili katika msikiti wa Kinondoni Muslim jijini Dar es Salaam kwa ajili ya Swala ya Idd Agosti 19, 2012

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein akisalimiana na watoto wa kiislamu walioshiriki katika Sala ya Iddi el Firti iliyowajumuisha waislamu kutoka mitaa mbali mbali katika Mji wa Zanzibar na kusaliwa Kitaifa katika Msikiti wa Mwembeshauri Mjini Zanzibar. Picha na Ramadhan Othman IKulu]

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein (wa tano kushoto) akijumuika na Waislamu wananchi na Viongozi mbalimbali katika Sala ya Iddi El Fitri iliyosaliwa Kitaifa katika Msikiti wa Mwembeshauri Mjini Zanzibar [Picha na Ramadhan Othman IKulu]

Mama Salma Kikwete akipeana mkono wa Iddi na kinamama waliohudhuria Swala ya Iddi Agosti 19, 2012 katika msikiti wa Kinondoni Muslim jijini Dar es Salaam.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein akiwa katika Baraza la Iddi El Fitri Zanzibar