Maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru; Mwelekeo wa BRELA

The Zanzibar President Dr Mohamed Shein (left) shares light moment withe Deputy Registrar-Commercial Laws, Andrew Mkapa (right) at the ongoing 50th Anniversary of Independence exhibition in the Mwalimu JK Nyerere fair grounds along Kilwa road Dar es Salaam. PHOTO/DAMAS MWITA.

Na Damas Mwita
Sabasaba-Dar es Salaam

Katika Kuadhimisha Miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara, Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara wamejivunia kuondoa urasimu katika utoaji wa huduma zake kutoka muda usiojulikana hadi kufikia siku moja hadi tatu kwa usajili wa majina ya biashara na siku tatu mpaka tano kwa usajili wa makampuni.

Akielezea mafanikio hayo, Afisa Mtendaji Mkuu wa BRELA, Esteriano Mahingila, amesema wakala inalenga kuboresha huduma zake kuwa za kisasa kwa kutumia teknohama ili kuweza kumhudumia mteja popote alipo.

Kwa minajiri hiyo BRELA inaendelea na programu ya kuweka nyaraka zake zote kwenye mifumo ya kielektroniki, kuimarisha kitengo cha utaalamu wa mawasiliano na kompyuta, kuimarisha zana za kutendea kazi, ili kuimarisha uwezo wa wakala kutimiza azma yake ya kuwa na huduma za kimataifa kulingana na dira yake.

Wakala pia inalenga kuwa na jengo lake ili kuboresha zaidi huduma zitolewazo na wateja waweze kuifikia wakala kwa urahisi.