
Baadhi ya watoto waliopata daraja la ‘comunio’ wakiwa katika ibada jana Kanisa Kuu Katoliki la Jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya walimu (mstari wa pili kutoka mbele) waliowaandaa wanafunzi kupata daraja la ekaristi takatifu wakiwa katika ibada hiyo.
ASKOFU Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo jana aliongoza ibada maalumu ya kutoa daraja la ‘comunio’ kwa takribani watoto 54 wa Parokia ya Mtakatifu Joseph ya jijini Dar es Salaam.
Misa hiyo ambayo pia ilihudhuriwa na Paroko, Padri Joseph Masenge ilifanyika katika Kanisa Kuu la St. Joseph na kuhudhuriwa na mamia ya waumini wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la jijini Dar es Salaam.

ASKOFU Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo akipokea vipaji katika ibada hiyo.