Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Hussein Mwinyi (kushoto) na Naibu Waziri Dk. Seif Rashid (kulia) wakijiandaa kuondoka katika ukumbi wa mikutano wa wizara hiyo mara baada ya kumaliza kuongea na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya siku ya wachangia damu Duniani yatakayofanyika kitaifa mkoani Kilimanjaro tarehe 14 Mwezi huu. Uchangia damu wa hiari umeongezeka toka chupa 52,000 kwa mwaka 2005 na kufikia chupa 140,000 kwa mwaka 2011, kauli mbiu ya mwaka huu ni “kila mchangia damu ni shujaa”. Picha na Anna Nkinda - Maelezo