Maadhimisho Siku ya Mtoto wa Afrika: Viongozi wa Dini Wakemea Ukatili

Mwakilishi kutoka Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), Sheikh Shomari Mchongoma (kushoto) akizungumza katika mkutano wa vyombo vya habari pamoja na viongozi wa dini kutoka BAKWATA, Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) na Mtaalamu wa Saikolojia ya Jamii, John Ambrose kukemea vitendo vya kikatili dhidi ya watoto, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika.

 

Ofisa Miradi wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA), Godfrida Jola (kulia) ambaye alimwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo akizungumza katika mkutano wa vyombo vya habari ulioandaliwa na kushirikisha viongozi wa dini kutoka Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) na Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) kukemea vitendo vya kikatili dhidi ya watoto, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika. Kutoka kushoto ni Sheikh Shomari Mchongoma (BAKWATA), Bw. Lucas Singili (CCT), pamoja na Mtaalamu wa Saikolojia ya Jamii, John Ambrose.

 

Mwakilishi kutoka Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), Bw. Lucas Singili (katikati) akizungumza katika mkutano wa pamoja na viongozi wa dini kutoka BAKWATA, CCT na Mtaalamu wa Saikolojia ya Jamii, John Ambrose kukemea vitendo vya kikatili dhidi ya watoto, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika. Mkutano huo uliandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA). Kulia ni Mtaalamu wa Saikolojia ya Jamii, John Ambrose na Sheikh Shomari Mchongoma wa BAKWATA (kushoto).

 

VIONGOZI wa Dini wamekemea vitendo vya ukatili kwa watoto na kwani vimekemewa hata katika vitabu vya dini, huku wakimtaka kila mmoja kumlinda mtoto pamoja na kueneza elimu ya malezi. Viongozi hao walioshiriki katika mkutano wa vyombo vya habari ulioandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA) kutoka Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) na Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) kwa pamoja waliungana na TAMWA kukemea vitendo vya kikatili wanaofanyiwa watoto, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika.

Akizungumza Mwakilishi kutoka Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), Sheikh Shomari Mchongoma alisema jamii kwa pamoja inapaswa kuungana na kukemea vitendo vya kikatili kwani ni kinyume cha imani zetu. Alisema jambo pekee ambalo linaweza kufanikisha mapambano hayo ni jamii kumrudia mwenyezi Mungu na kukemea vitendo viovu anavyochukizwa navyo.

“…Wakati umefika tuangalie ni namna gani kumkomboa mtoto wetu kwenye wimbi la mateso ya kikatili ambayo wamekuwa wakitendewa baadhi ya watoto wetu. Mtoto anaweza kuwa salama endapo tutaungana na kukemea vitendo hivyo bila kujali tofauti zetu,” alisema Sheikh Mchongoma.

Kwa upande wake, Mwakilishi kutoka Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), Bw. Lucas Singili alisema mtoto anaitaji malezi ya pamoja kwa ushirikiano ikiwa ni kuwaweka karibu ili waweze kukua katika malezi mema. Watoto hawapaswi kutengwa wala kufanyiwa vitendo vya kikatili zaidi ya kuwapa msaada kutoka kwa wazazi, walezi na jamii kwa ujumla ili waweze kuwa raia wema wenye maadili katika taifa la baadaye.

 

Mtaalamu wa Saikolojia ya Jamii, John Ambrose (wa kwanza kulia) akizungumza katika mkutano wa pamoja na viongozi wa dini kutoka BAKWATA, CCT kukemea vitendo vya kikatili dhidi ya watoto, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika. Mkutano huo uliandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA). Wengine kushoto ni viongozi wa dini.

 

Mtaalamu wa Saikolojia ya Jamii, John Ambrose (kulia) akizungumza katika mkutano wa pamoja na viongozi wa dini kutoka BAKWATA, CCT kukemea vitendo vya kikatili dhidi ya watoto, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika. Kulia ni Ofisa Miradi wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA), Godfrida Jola akifuatilia mazungumzo hayo.

 

Sehemu ya wanahabari na maofisa wa TAMWA wakiwa katika mkutano huo.

 

Aidha aliongeza kuwa mtoto hapaswi kuchokozwa kwa nmna yoyote kama wanavyofanyiwa ukatili na mambo yasio mema na baadhi ya watu.Alisema hata vitabu vya dini vimekemea aina yoyote ya uchokozi dhidi ya watoto, hivyo kuiomba jamii kushirikiana katika kutoa elimu ya malezi mema kwa watoto waje kuwa raia wema na bora baadaye. “…Mtoto achokozwi, usimchokoze mtoto hata maandiko ya dini yanasema hivyo…,” alisisitiza Bw. Singili wa CCT.

Naye Mtaalamu wa Saikolojia ya Jamii, John Ambrose akizungumza na wanahabari katika mkutano huo, alisema yapo madhara makubwa yanayomtokea mtoto endapo akipitia katika vitendwa vya unyanyasaji. Alisema mtoto anapokumbana na vitendo vya unyanyasaji anapoteza matumaini kwa jamii, anapoteza imani, anajenga hofu na thamani yake inashuka hivyo kuishi katika maisha mabaya zaidi.

Alieleza kuwa, mtoto anayefanyiwa vitendo vya kikatili asipo badilishwa huenda akawa mkatili zaidi hapo baadaye jambo ambalo tunaweza kujikuta tunaandaa taifa hatari, hivyo kumtaka kila mmoja katika nafasi yake kukemea vitendo vya kikatili dhidi yao ili kumlinda mtoto.