LUTENI Kanali Issac Zida amechaguliwa na viongozi wa Jeshi la Bukina Faso kuiongoza nchi hiyo kuelekea katika taratibu za kufanya uchaguzi. Baada ya kutoka kwa maamuzi hayo ya Jeshi sasa yameondoa sitofahamu iliyokuwepo ya kwamba ni nani atakaye mrithi Rais Blaise Campaore ambaye alijiuzulu kwa nguvu za wananchi kufuatia maandamano ya kumpinga yalioambatana na vurugu kubwa.
Luteni Kanali Zida tayari ametoa hotuba yake katika runinga kutangaza kwamba amechukua mamlaka kuiongoza nchi hiyo katika uongozi wa mpito. Hatua hiyo inaonekana kutofautiana na ile ya mkuu wa jeshi Jenerali Honore Traore ambaye alijitangaza kuwa kiongozi mpya mda mfupi baada ya kujiuzulu kwa Campaore.
Hatahivyo Sahihi ya Jenerali Honore Traore ilikuwa katika taarifa iliosomwa na Luteni kanali Issac Zida ambaye inadaiwa alichaguliwa na wakuu wote wa jeshi kuongoza.
-BBC