Lusekelo Mwaseba Ateuliwa Naibu Kamishna Mkuu TRA

Lusekelo Mwaseba

Lusekelo Mwaseba


RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana Lusekelo Mwaseba kuwa Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). Taarifa iliyotolewa Ikulu, Dar Es Salaam, Oktoba Mosi, 2014, na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, imesema kuwa uteuzi huo unaanza leo. Kabla ya uteuzi wake, Mwaseba alikuwa Kamishna wa Uchunguzi katika Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).