LUKUVI Atoa Pikipiki 16 Kwa Makatibu wa CCM Isimani

Katibu wa CCM mkoa wa Iringa Hassan Mtenga  akijaribu moja kati ya  pikipiki 16  zilizotolewa na mbunge wa jimbo la Ismani Wiliam Lukuvi kwa makatibu kata wa CCM jimboni kwake kwa ajili ya kusaidia usafiri  ofisi za kata

Katibu wa CCM mkoa wa Iringa Hassan Mtenga akijaribu moja kati ya pikipiki 16 zilizotolewa na mbunge wa jimbo la Ismani Wiliam Lukuvi kwa makatibu kata wa CCM jimboni kwake kwa ajili ya kusaidia usafiri ofisi za kata

Makatibu kata wa CCM jimbo la Isimani wakiwa wamezunguka pikipiki 16 zilizotolewa na mbunge wao Wiliam Lukuvi kwa ajili ya  kuwasaidia katika shughuli za kila siku
makatibu kata na katibu wa wilaya  ya Iringa  wakishangilia  wakati katibu wa mkoa wa Iringa Hassan Mtenga akijaribu pikipiki hizo
katibu  wa mbunge wa jimbo la Isimani Bw  Thom Malenga  kushoto akimkabidhi simu 16  zilizotolewa pamoja na pikipiki 16  na mbunge Lukuvi  kwa ajili ya makatibu wa CCM kata
Katibu   wa CCM mkoa  wa Iringa Hassan Mtenga akikabidhi simu kwa katibu kata wa CCM jimbo la Isimani
 Na MatukiodaimaBlog
MBUNGE
wa jimbo la Isimani Bw Wiliam Lukuvi emekabidhi msaada wa pikipiki 16
zenye thamani ya zaidi ya Tsh milioni 22 makatibu kata wote 16  wa chama
cha mapinduzi (CCM )katika  jimbo hilo la Isimani wilaya ya  Iringa
vijijini   ili kuwawezesha kufanya kazi ya chama kiufanisi  zaidi .
 
Akikabidhi
msaada  huo pikipiki  na simu 16 leo kwa makatibu hao wa kata kwa niaba ya
mbunge Lukuvi ,katibu wa CCM mkoa wa Iringa Bw Hassan Mtenga  alisema
kuwa mkoa wa Iringa una  zaidi ya  wabunge wa watano wanaotokana na
chama cha CCM  ila hajapata  kuona  mbunge anayewajali makatibu wa chama
kama  alivyofanya mbunge huyo wa  jimbo la Isimani na kuwa kufanya
hivyo  ni  kuongeza ushindi wa CCM .
 

katika  mkoa  wetu  wa Iringa tunaowabunge wa CCM lakini  toka
wameanza  mbaka wanamaliza  hawajapata  kutoa msaada kama  huo  ila
Lukuvi  si tu anaanza leo tuseme ni  muendelezo kwa   ni mara kwa mara
amekuwa jirani na chama  kwa  kusaidia  makatibu hao usafiri  wa
pikipiki na kuwa  hii ni mara ya pili anatoa msaada  huo wa pikipiki
baada ya  zile za awali  kuchakaa”
 
Bw
Mtenga  alisema  kuwa Lukuvi amekuwa ni mbunge na kiongozi  wa aina
yake  kwani amekuwa ni msaada mkubwa  zaidi ndani ya chama na hata
serikalini kutokana na utendaji kazi wake na  hivyo mbali ya  kuwa si
wakati muafaka sana ila  yeye kama katibu wa CCM mkoa wa Iringa
anatambua mchango mkubwa na heshima kubwa ambayo mbunge Lukuvi
ameonyesha ndani ya chama na katika  jimbo lake la Isimani kwa
kutekeleza ilani  vizuri na hivyo kuwataka makatibu hao na  wana CCM
jimbo la Isimani kuendelea kutoa ushirikiano kwa mbunge wao.
 

Mimi  ni katibu  wa CCM mkoa hivyo natamka  wazi  kuwa mbunge   Lukuvi
aendelee kuwa mbunge wa  jimbo la Isimani kwani ni mbunge anayetambua
changamoto za  watendaji  wake na  wananchi waliomchagua na kuzitatua na
ndio jambo ambalo chama kinahitaji kwa  wabunge  wake  kuzifanya “
 
Katibu
wa CCM wilaya ya Iringa Bw Andrew Kashililika alisema kuwa msaada  huo
wa  piki piki katika jimbo la Isimani ni msaada  mkubwa  zaidi kwani
hali ya  usafiri kwa makatibu wa CCM kata  bila jitihada za mbunge  huyo
hali ya utendaji kazi kwao  ingekuwa ngumu  zaidi.
 
katibu
huyo  alisema ushindi ambao  CCM iliupata katika uchaguzi wa Serikali
za mitaa kwa CCM kushinda  zaidi ya asilimia 90n katika wilaya  hiyo ya
Iringa  vijijini ni wazi katika  uchaguzi mkuu utakaofanyika Octoba
mwaka huu CCM kitaibuka na ushindi  wa  kishindo zaidi .
 
Kwa
upande  wake  katibu  wa ofisi ya mbunge Lukuvi Bw Thom Malenga
alisema  kuwa  ofisi ya mbunge  ilipokea barua za maombi kutoka kwa
makatibu hao wa CCM kata  kuomba  kupewa  pikipiki mpya  baada ya  zile
za awali kuchakaa na  hivyo kukwamisha  utendaji kazi wao .
 
Alisema
kuwa  baada ya hapo  ndipo  Lukuvi alipoamua  kutafuta  pesa kiasi cha
Tsh milioni 26 kwa ajili ya kununua pikipiki  hizo na kuwapa mawasiliano
ya simu baada ya  kuwa  sehemu kubwa ya  jimbo  hilo kuwa na
mawasiliano ya  simu na kutokana na kuwa na vitendea kazi vya
mawasiliano itawawezesha kufikisha taarifa  kwa haraka katika  makao
makuu ya  chama.
 
Hata
hivyo  aliwataka makatibu kata  hao kujaribu  kuwa waangalifu  katika
kutumia pikipiki  hizo ili  kuepuka kuwasababishia ajali kwani bila
uangalifu katika matumizi  upo  uwezekano wa badala ya  kufurahia
msaada  huo wakaishia  kujutia  majeraha yatakayotokana na wao kutokuwa
makini.
 
Bw
Zacharia Kitule katibu kata  wa CCM kata ya Nyang’oro  akishukuru  kwa
niaba ya  wenzake kwa msaada  huo alimpongeza mbunge Lukuvi kwa
kuwamsikivu na kutimiza kila anachoahidi kwa  wakati zaidi na kuwa wao
kama makatibu kata wapo tayari  kuendelea  kutoa ushirikiano zaidi
kwake  ili kuona anaendelea  kuwa mbunge wa  jimbo hilo hadi hapo
atakapoamua  kustaafu mwenyewe.