Lukaku Aipeleka Ubelgiji Robo Fainali EURO

160610140401_lukaku_624x351_ap_nocredit

Romelu Lukaku alifunga mabao mawili huku timu ya taifa la Ubelgiji ikipata ushindi wake wa kwanza katika michuano ya Euro2016 na kuharibu fursa ya timu ya Jamhuri ya Ireland kufika robo fainali.

Baada ya kukamilika kwa kipindi cha kwanza ambapo hakuna timu ilioona lango la mwengine,Lukaku aliifungia Ubelgiji bao la kwanza baada ya kupata pasi muruwa.

Baadaye Axel Witsel alifunga bao la pili kupitia kichwa katika dakika ya 61,kabla ya Lukaku kufunga bao la tatu baada ya kushambulia ngome ya Ireland.

Timu ya Jamhuri ya Ireland ilishindwa kufanya mashambulio katika ngome ya Ubelgiji