Balozi wa Denmark nchini Tanzania, Einar H. Jensen (kulia) akimkabidhi mmoja wa wawakilishi wa mikoa wa mashirika washauri wa msaada wa kisheria laptop kwa niaba ya taasisi yake. Msaada huo ulitolewa na Mfuko wa Fedha za Msaada wa Kisheria (LSF) unaofadhiliwa na Shirika la DANIDA la nchini Denmark na Shirika la DFID kutoka Uingereza. Kushoto ni Mjumbe wa Bodi ya LSF, Joseph Ndungulu akishuhudia.
Mshauri Kiongozi wa DFID Tanzania, Helen Barnes (kulia) akimkabidhi mmoja wa wawakilishi wa mikoa wa mashirika washauri wa msaada wa kisheria laptop kwa niaba ya taasisi yake. Msaada huo ulitolewa na Mfuko wa Fedha za Msaada wa Kisheria (LSF) unaofadhiliwa na Shirika la DANIDA la nchini Denmark na Shirika la DFID kutoka Uingereza. Katikatika ni Mjumbe wa Bodi ya LSF, Joseph Ndunguru akishuhudia.
Mjumbe wa Bodi ya LSF, Dk. Benson Bana (kulia) akimkabidhi mmoja wa wawakilishi wa mikoa wa mashirika washauri wa msaada wa kisheria laptop kwa niaba ya taasisi yake. Msaada huo ulitolewa na Mfuko wa Fedha za Msaada wa Kisheria (LSF) unaofadhiliwa na Shirika la DANIDA la nchini Denmark na Shirika la DFID kutoka Uingereza. Katikati akishuhudia ni, Mjumbe wa Bodi ya LSF, Joseph Ndungulu.
Balozi wa Denmark nchini Tanzania, Einar H. Jensen akizungumza katika hafla ya Mfuko wa Fedha za Msaada wa Kisheria (LSF) kuwakabidhi wawakilishi wa mikoa wa mashirika washauri wa msaada wa kisheria laptop kwa niaba ya taasisi zao zinazotoa msaada wa kisheria kwa jamii.
Mshauri Kiongozi wa DFID Tanzania, Helen Barnes akizungumza katika hafla ya Mfuko wa Fedha za Msaada wa Kisheria (LSF) kuwakabidhi wawakilishi wa mikoa wa mashirika washauri wa msaada wa kisheria laptop kwa niaba ya taasisi zao zinazotoa msaada wa kisheria kwa jamii.
Mjumbe wa Bodi ya LSF, Dk. Benson Bana akizungumza katika hafla ya Mfuko wa Fedha za Msaada wa Kisheria (LSF) kuwakabidhi wawakilishi wa mikoa wa mashirika washauri wa msaada wa kisheria laptop kwa niaba ya taasisi zao zinazotoa msaada wa kisheria kwa jamii.
Baadhi ya laptop zilizotolewa kwa wasaidizi hao wa kisheria kwa jamii.
Viongozi hao wakiwa katika hafla hiyo leo jijini Dar es Salaam.
Mjumbe wa Bodi ya LSF, Joseph Ndunguru (kulia) akimkabidhi mmoja wa wawakilishi wa mikoa wa mashirika washauri wa msaada wa kisheria laptop kwa niaba ya taasisi yake. Msaada huo ulitolewa na Mfuko wa Fedha za Msaada wa Kisheria (LSF) unaofadhiliwa na Shirika la DANIDA la nchini Denmark na Shirika la DFID kutoka Uingereza.
MFUKO wa Fedha za Msaada wa Kisheria (LSF) umekabidhi laptop 170 kwa asasi mbalimbali zinazotoa msaada wa kisheria kwa wananchi wahitaji katika mikoa anuai nchini Tanzania.
Akizungumza kabla ya kukabidhi vitendea kazi hivyo kwa wawakilishi wa mikoa wa mashirika washauri wa msaada wa wa kisheria, Mjumbe wa Bodi ya LSF, Dk. Benson Bana aliwataka sema shirika hilo linaamini zitatumika katika kutatua changamoto anuai kwa asasi husika ikiwa ni chachu ya kuongeza ufanisi kwa kazi zao.
Laptop hizo 170 zimekabidhiwa leo jijini Dar es Salaam na Balozi wa Denmark nchini Tanzania, Einar H. Jensen huku akizitaka asasi hizo muhimu kuendelea kuisaidia jamii inayoitaji msaada wa kisheria popote walipo kwani zipo familia hasa wajane wanaitaji na wanashindwa namna ya kupata.
LSF ni mfuko huru wa msaada wa kisheria unaotoa msaada kwa mashirika watoa msaada wa kisheria, kitaasisi na kiufundi ili kuongeza uwazi na uwajibikaji katika sekta ya sheria chini ya ufadhili wa Shirika la DANIDA la nchini Denmark na Shirika la DFID la Uingereza.
Afisa Ufuatiliaji na Matokeo wa Mfuko wa Fedha za Msaada wa Kisheria (LSF), Saada Mkangwa (kushoto mbele) akiwasilisha mada ya kuwajengea uwezo wawakilishi wa mikoa wa mashirika washauri wa msaada wa kisheria leo jijini Dar es Salaam.
Meneja Ufuatiliaji na Matokeo wa Mfuko wa Fedha za Msaada wa Kisheria (LSF), Said Chitong (kulia) akiwasilisha mada ya kuwajengea uwezo wawakilishi wa mikoa wa mashirika washauri wa msaada wa kisheria leo jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya wawakilishi wa mikoa wa mashirika washauri wa msaada wa kisheria wakiwa katika semina ya kuwajengea uwezo.