• Aliumia zaidi wananchi walipolia
• Asema muda ukifika atasema cha kufanya
• Chadema watamba kushinda Igunga
Na Maregesi Paul, Dodoma
Babu sikutarajia kama hali hiyo ingelitokea,” alisema Lowassa. Alipotakiwa kusema yeye atajiuzulu lini kwa kuwa naye ni miongoni mwa wana CCM ambao wamekuwa wakilalamikiwa, alisema kwa kifupi kwamba muda ukifika nitasema.
Wakati huo huo, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimeramba kitashinda uchaguzi mdogo katika jimbo hilo. Majigambo hayo yalitolewa bungeni jana na Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, Kabwe Zitto muda mfupi baada ya kipindi cha maswali na majibu.
Kabla ya Zitto kuzungmzia jimbo hilo, aliomba mwogozo wa Spika akitaka kujua kama kiongozi huyo wa Bunge amekwisha kupata taarifa za Rostam kujiuzulu. “Mheshimiwa Spika, ndani ya Bunge lako tukufu kuna kiti cha jimbo moja kiko wazi, naomba ulieleze Bunge lako kama pia umeshaijulisha Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuhusu jambo hili. “Kama kama kiti hicho kiko wazi, twambie ili tujiandae tukachukue Jimbo letu la Igunga,” alisema Zitto na kukaa.
Akijibu hoja hiyo, Spika wa Bunge, Anne Makinda alisema hana taarifa rasmi za jimbo hilo kuwa wazi na kwamba akipata taarifa hizo rasmi atalitangazia Bunge. Spika alisema nay eye alisikia na kuzisoma taarifa hizo katika vyombo vya habari tu.
“Ukitaka kuona watu wanavyotaka kupoteza muda ndiyo kama hivi, lakini, hata sisi tumeona katika mitandao kama mlivyoona nyinyi. “Binafsi mheshimiwa hajaniandikia barua kunijulisha hili, nitajulishwa na mamlaka husika na nikipata maelezo nitatoa taarifa,” alisema Spika Makinda.
Rostam alijiuzulu ubunge wa jimbo hilo oamoja na ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM akiwakilisha Mkoa wa Tabora mjini Igunga juzi. Alikuwa akizungumza na wazee na viongozi wa CCM wa Wilaya ya Igunga, mkoa wa Tabora na wa baadhi ya mikoa jirani.
Pamoja na mambo mengine, alisema amechukua uamuzi huo ili kuepukana na siasa uchwara na za kuchafuana zinazoendeshwa ndani ya CCM hivi sasa. Alisema kwa sasa atajikita katika biashara zake kwa kuwa yeye ni mfanyabiashara wa kimataifa.
Rostam ambaye ameliongoza jimbo hilo kwa miaka 18 alisema ataendelea kuwa mwanachama mwaminifu wa CCM.
Katika kikao hicho cha juzi baadhi ya wanachama na viongozi wa CCM walilia wakimsihi abadilishe uamuzi wake, huku wengine wakizimia kwa tamko lake la kujiuzulu.
Source: Mtanzania