Lowassa Azindua Maonesho ya Miaka 10 ya VICOBA Dar

Mjumbe wa Kamati ya VICOBA Tanzania, Magreth Mapunda (kushoto) akikabidhi Risala hiyo kwa Mgeni Rasmi, Edward Lowassa.

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akisalimiana na Mratibu wa Maonyesho ya VICOBA Tanzania,Aldo Mfinde wakati alipokuwa akiwasili kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar tayari kwa Uzinduzi rasmi wa maonyesho ya VICOBA Tanzania.Wa pili Kulia ni Naibu Waziri wa Kazi na Ajira,Mh. Makongoro Mahanga na Kulia ni Mwenyekiti wa CCM,Wilaya ya Ilala,Mh Assaa Simba.
Mratibu wa Maonyesho ya VICOBA Tanzania,Aldo Mfinde akizungumza machache wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Maonyesho ya Miaka Kumi ya Wafanya biashara ndogo ndogo na Wajasiliamali
wa  VICOBA uliyofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar
es Salaam.wa Tatu kulia ni Mgeni Rasmi katika uzinduzi huo,Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa.Wengine ni Naibu Waziri wa Kazi na Ajira,Mh. Makongoro Mahanga (pili kulia) na Mwenyekiti wa CCM,Wilaya ya Ilala,Mh Assaa Simba.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa (kulia) akimpongeza Mratibu wa Maonyesho ya VICOBA Tanzania,Aldo Mfinde mara baada ya kumaliza kuitambulisha Kamati ya VICOBA Tanzania iliokuwepo viwanjani hapo.
Burudani ya Ngoma za Asili.
Mjumbe wa Kamati ya VICOBA Tanzania,Bi. Magreth Mapunda akisoma Risala ya Chama chao hicho mbele ya Mgeni Rasmi,Mh. Edward Lowassa wakati wa hafla ya Uzinduzi rasmi wa Maonyesho ya Miaka Kumi ya Wafanyabiashara ndogo ndogo na Wajasiliamali
wa  VICOBA uliyofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar
es Salaam
leo.
Mjumbe wa Kamati ya VICOBA Tanzania,Bi. Magreth Mapunda (kushoto) akikabidhi Risala hiyo kwa Mgeni Rasmi,Mh. Edward Lowassa.
Mwenyekiti wa CCM,Wilaya ya Ilala,Mh Assaa Simba akisalimia Wanachama wa VICOBA Tanzania.
Naibu Waziri wa Kazi na Ajira,Mh. Makongoro Mahanga akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Mgeni Rasmi kuzungumza na Wanachama wa VICOBA.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akitoa hotuba yake mbele ya wanachama wa VICOBA Tanzania wakati hafla ya Uzinduzi wa Maonyesho ya Miaka Kumi ya Wafanya biashara ndogo ndogo na Wajasiliamali
wa  VICOBA uliyofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar
es Salaam
leo.Katika Hobuba yake,Mh. Lowassa aliwapongeza wana VICOBA kwa kuweza kujiajiri,kwani tatizo la ajira nchini bado ni tatizo kubwa na ni bomu linaweza kulipuka wakati wowote.Maonyesho hayo yataendelea mpaka jumamosi ijayo Oktoba 27.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa (kushoto) akiteta jambo na Naibu Waziri wa Kazi na Ajira,Mh. Makongoro Mahanga.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akicheza muziki sambamba na Wanachama wa VICOBA Tanzania wakati wa uzinduzi wa Maonyesho ya Biashara ya Miaka Kumi yam Wajasilia Mali wa VICOBA tangu kuanzishwa kwakwe,iliyofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akibonyeza kitufe kwenye kompyuta ikiwa ni ishara ya Uzinduzi rasmi wa Maonyesho ya Miaka Kumi ya Wafanya biashara ndogo ndogo na Wajasiliamali wa  VICOBA uliyofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar
es Salaam
leo.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiwapungia mkono Wanachama wa VICOBA wakati wa kuwaaga mara baada ya kufanya uzinduzi wa Maonyesho ya Miaka Kumi ya Wafanya biashara ndogo ndogo na Wajasiliamali
wa  VICOBA uliyofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar
es Salaam
leo.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa
akiagana na baadhi ya Wanachama wa VICOBA mara baada ya uzinduzi wa Maonyesho ya Miaka Kumi ya Wafanya biashara ndogo ndogo na Wajasilia mali wa  VICOBA uliyofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam
leo.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa
akiagana na Naibu Waziri wa Kazi na Ajira,Mh. Makongoro Mahanga.
Wanachama wa VICOBA wakijiburudisha kwa kucheza Muziki.
Maandamano ya Wanachama na Wajasiliamali wa VICOBA yakipita Mbele ya Mgeni Rasmi,ambaye ni Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa.