Lowassa Aifariji Familia ya Kusaga Msibani

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli, Edward Lowassa akimpa pole mfiwa, Mama Khadija Kusaga wakati alipofika nyumbani kwake Keko Maghorofani jijini Dar es Salaam jana.

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli, Edward Lowassa jana Jumapili jioni alikuwa ni miongoni mwa waombolezaji waliofika kuaga mwili wa Marehemu Sufiani Bakari Kusaga, Nyumbani kwake Keko Maghorofani jijini Dar es Salaam.

Marehemu Sufiani Bakari Kusaga alikuwa ni mume wa Mbunge wa zamani wa Jimbo la Temeke ambaye sasa hivi ni Katibu wa CCM Kishapu, Khadija Kusaga.

 

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli, Edward Lowassa akimfariji mfiwa, Mama Khadija Kusaga.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli, Edward Lowassa akiwa katika mazungumzo na Mbunge wa sasa wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu wakati walipokuwa kwenye msiba huo jana jioni.