Liverpool Yatinga Nusu Fainali EUROPA Ligi

33

Hatua ya Robo fainali ya michuano ya Europa imeendelea tena Alhamisi kwa michezo minne, ambapo Liverpool imefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali kufuatia ushindi wa mabao 4 -3 dhidi ya Borrussia Dortmund.

Magoli ya Liverpool yamefungwa na wachezaji Divock Origi, Philippe Coutinho, Mamadou Sakho na Dejan Lovren.

2

Na magoli ya Dortmund yamefungwa na Henrikh Mkhitaryan, Pierre-Emerick Aubameyang na Marco Reus .

Sevilla imeiondoa Athletic Bilbao kwa changamoto ya penalti 5-4 kufuatia sare ya jumla ya 3-3 baada ya kila timu kushinda 2-1 mechi ya nyumbani.

liv

Villarreal imeifunga Sparta Praga bao 4- 2 na Shakhtar Donetsk imeirarua Sporting Braga kwa mabao 4-0.

Kwa matokeo hayo Liverpool inaungana na Sevilla, Shakhtar Donetsk na Villarreal katika hatua ya nusu fainali