Liverpool Wapewa Kigogo wa Hispania EUROPA Ligi

europa

klabu ya Liverpool ya Uingereza imekabidhiwa Villarreal ya Uhispania katika hatua ya nusu fainali ya Europa Ligi.

Shakhtar Donetsk kutoka Ukraine nao watakutana na mabingwa watetezi Sevilla.

Liverpool v Villarreal
Shakhtar Donetsk v Sevilla

Liverpool walifika nusufainali kwa kulaza Borussia Dortmund Alhamisi kwenye mechi ya kusisimua wakitoka nyuma 2-0 wakati wa mapumziko na kushinda 4-3 uwanjani Anfield.Walifanikisha ushindi wa jumla wa 5-4.

Sevilla, ambao wanapigania kushinda kikombe kwa mara ya tatu mtawalia, walitinga nusufainali kwa kuwashinda Athletic Bilbao kupitia mikwaju ya penalti.