Liverpool na Manchester City hakuna mbabe.

Mario Balotelli alizawadiwa Kadi nyekundu katika mcheo huo

Bao la kujifunga la Joleon Lescott lilifuta jitihada za awali za Vincent Kompany kufunga bao wakati Manchester City walipoongeza wigo wa pointi hadi tano wakiendelea kusalia kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya Kandanda ya England.
Liverpool yatoka sare na Manchester City bao 1-1
Mario Balotelli alitolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kuoneshwa kadi mbili za manjano katika kipindi cha dakika 17 tangu alipoingia kuchukua nafasi ya Samir Nasri.
Lakini Manchester City, ambao wamepoteza pointi kwa mara ya pili waliambulia sare ya kufungana bao 1-1.
Mshambuliaji wa Liverpool ambaye pia huchezea timu ya taifa ya Wales Craig Bellamy hakucheza mechi hiyo kufuatia kifo cha meneja wa Wales Gary Speed.
Swansea na Aston Villa walitoka sare ya kutofungana katika mchezo wa awali ambao uligubikwa kwa kiasi kikubwa na kifo cha meneja wa Wales Gary Speed.
Speed, alikutwa amekufa nyumbani kwake Cheshire asubuhi ya siku ya Jumapili.
Mechi hizo mbili zilianza kwa kimya cha dakika moja kutoa heshima kwa Gary Speed na huko Swansea mashabiki walipiga kofi huku wakiimba “kulikuwa na Gary Speed mmoja tu”.
Leroy Lita aliikosesha nafasi mbili murua za kufunga mabao timu ya Swansea.
Alifumua mkwaju mkali zikiwa zimesalia dakika 20 kabla mchezo kumalizika uliookolewa na mlinda mlango wa Aston Villa Shay Given, kabla ya mlinda mlango huyo kuokoa tena mpira kutoka miguuni mwa Lita.

-BBC