Kwa mara ya kwanza tangu kuasisiwa kwa ligi kuu ya Uingereza ,thamani ya uuzaji na malipo ya wachezaji,umegonga pauni bilioni moja. Pauni milioni £965m zilitumika msimu uliopita wa mwaka wa 2014-15
Vilabu 20 vya ligi ya premia vimetumia takriban pauni milioni £130 kuanzia Januari mosi-31.
• Ligi ya pauni bilioni moja £1 bilioni
Gharama ya kununua wachezaji katika dirisha la uhamisho la ligi ya Premia mwaka 2015/16
o £130 milioni pesa zilizotumika katika dirisha dogo la Januari
o £29m Kiwango kilichotumiwa na klabu ya Newcastle United
Newcastle imewanunua Jonjo Shelvey, Andros Townsend na Henri Saivet.
Vilevile timu hiyo imeweka dau ya paundi milioni £21m kwa ajili ya kununua huduma za mshambulizi wa West Brom Saido Berahino.
Afsa mmoja wa kampuni ya urasimu ya Sports Business Group at Deloitte, Dan Jones, amesema kuwa ” kwa mara nyengine tumeshuhudia vilabu vinavyoshiriki ligi kuu ya uingereza vikiwekeza kiasi kikubwa mno cha fedha ilikusajili ufundi na huduma za wachezaji.”
“Hii ndio mara ya kwanza kwa thamani ya uhamisho kuzidi pauni bilioni moja”
Newcastle United wamewasilisha ombi la £21m la kutaka kumnunua mshambuliaji wa West Brom Saido Berahino.
Meneja wa West Brom Tony Pulis alisema Berahino, 22, “amepoteza
miezi mitatu au mme” baada yake kuzuiwa kuhamia Tottenham Agosti mwaka uliopita.
Mshambuliaji huyo alionekana kusema kwamba hangechezea mwenyekiti wa West Brom Jeremy Peace tena baada yake kuzuiwa kuhama.
Berahino alianza mechi, jambo ambalo limekuwa nadra sana kwake, mechi dhidi ya Peterborough katika Kombe la FA Jumamosi na akawafungia mabao mawili na kuwasaidia kutoka sare ya 2-2.
Mabao hayo yalifikisha jumla ya mabao aliyofunga msimu huu hadi sita.
Msimu uliopita, amefungia West Brom mabao 22 ligini kwa jumla.
“Kuna siku nyingine mbili za kusubiri,” alisema Pulis baada ya mechi dhidi ya Peterborough Jumamosi.