Ligi Daraja La Pili Kuendelea Leo, Pata Msimamo Hapa

sdl

Ligi Daraja la Pili (SDL) inatarajiwa kumalizika wikiendi hii kwa michezo 12 kuchezwa katika makundi ya A, B, C & D katika viwanja mbalimbali nchini, huku kila kundi likitoa timu moja ya juu itakayocheza fainali za kupanda ligi daraja la kwanza msimu ujao.

Leo Jumamosi Kundi C, Alliance Schools watakua wneyeji wa Bulyankulu katika uwanja wa CCM Kirumba, JKT Rwamkoma watacheza dhidi ya Pamba FC uwanja wa Karume Musoma, na Madini FC watakua wenyeji wa AFC Arusha uwanja wa Mbulu.

Kundi D, Jumapili Mkamba Rangers watacheza dhidi ya Wenda FC uwanja wa CCM Mkamba, Sabasaba watakua wenyeji wa The Mighty Elephant uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, huku Mbeya Warriors wakicheza dhidi ya African Wanderes katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

Timu moja ya kwanza kutoka katika kila kundi zitacheza hatua ya Fainali Machi 7-14, 2015 uwanja wa Karume jijini Dar es salaam, ili kupata timu tatu za juu zitakazopanda moja kwa moja ligi daraja la kwanza (StarTimes League) msimu ujao.
Kupata msiammo wa Ligi Daraja la Pili (SDL) fuata link hii http://tff.or.tz/league/tff-league/18-second-division-league