MAELFU ya watu walikusanyika katika miji miwili mikubwa nchini Libya, yaTripoli na Benghazi Februari 15, 2013 kusherehekea miaka miwili tangu kuanza kwa mapinduzi yaliyosababisha kuangushwa kwa Moammar Gaddafi.
Katikati ya jiji la Tripoli, mamia yawatu walikusanyika katika uwanja wa mashahidi, wakipepea bendera na maputo na kuimba nyimbo za kusifu mashahidi waliokufa katika mapinduzi ya Libya wakati magari yakipita mjini wakipiga honi.
Mjini Benghazi, mji wa mashariki ambako ulianzia uasi, maelfu yawatu waliandamana katika njia ile ileya maandamano yaliyofanyika Februari 15, mwaka 2012, kichocheo ambacho kilizusha vuguvugu la mapinduzi siku mbili baadaye.
Waandamanaji wa Benghazi pia waliwasifu mashahidi, pamoja na wale ambao wamepotea na wale ambao wamejeruhiwa katika mzozo ambao ulidumu kwa zaidi ya miezi minane hadi pale alipouwawa kanali Gaddafi Oktoba 20, mwaka 2011. Lakini waandamanaji pia wamekosoa viongozi wapya, wakidai hususan kugawana zaidi madaraka.
Serikali tayari imechukua hatua madhubuti za kudhibiti jaribio lolote la waungaji mkono wa utawala wazamani kufanya fujo huku waandamanaji wakiwa na hasira wanawashutumu watawala wapya kwa kushindwa kuleta mabadiliko.
Baadhi yawakosoaji wa serikali wamediriki hata kutoa wito wa mapinduzi mapya, wakati wakishutumu madaraka ya wanamgambo wa zamani ambao walisaidia kufikisha mwisho utawala wa kanali Gaddafi wa zaidi ya miongo minne.
People celebrate Libya’s liberation in Misrata on Oct. 23, 2011, after the death of former leader Muammar Gaddafi. Gaddafi’s body was temporarily displayed in the western Libyan city. Sherehe mjini Tripoli kusherehekea miaka miwili tangu kuondolewa utawala waGaddafi
Wakati huo huo viongozi wa makundi yanayotaka kupata utawala wa ndani waeneo la mashariki ya Libya wamefuta maandamano yaliyopangwa kutokana na hofu za kutokea ghasia jana ijumaa, wakati maelfu yawatu waliingia mitaani kuadhimisha miaka miwili tangu kuanza kwa vuguvugu la mapinduzi nchini humo.
Makundi mjini Benghazi, yanayojita, vuguvugu la mapinduzi ya mwaka 2011 ambayo yalimuondoa kanali Gaddafi kutoka madarakani, yalitayarisha maandamano makubwa kudai usalama zaidi na uwekezaji katika mji huo wa pili kwa ukubwa nchini Libya.
Hali ilikuwa ya mchanganyiko baina yawale waliokuwa wakiimba kwa furaha na kupunga bendera na wale waliokuwa wakiimba wimbo wa taifa, nyuso zao zilipakwarangi ya bendera ya Libya, na wale ambao walikuwa wamesimama tu wakutumbua macho bila kuonyesha hisia yoyote.
-DW